Bondia Hassan Mwakinyo 'Champez' ameweka wazi kuwa kwa sasa mipango yake ni kutafuta mapambano ya kimataifa sanasana kucheza kwenye majukwaa na mapambano makubwa nchini Marekani na hana kabisa mipango ya kucheza pambano lolote Tanzania
Mwakinyo amesema
"Nipo huku najifua lakini na kufanya mipango mengine ila sitarajii na wala sina mkakati wowote ambao utanifanya nipande ulingoni nchini Tanzania kwa sababu kwa sasa focus yangu na ndoto yangu ni ya kuweza kupata nafasi ya kucheza mapambano nchini Marekani."
Kwa kipindi cha mwezi sasa Mwakinyo yupo zake nchini Marekani akijifua katika gym mbalimbali maarufu ikiwemo gym ya "5th St Gym" ambayo aliwahi pia kupita bondia maarufu Mohamed Ally,lakini pia Mwakinyo siku za hivi karibuni ameonekana kwenye video akiwa mazoezini akipewa mbinu na bondia mkubwa duniani Bernard Hopkins ambaye kwasasa amestaafu ndondi.
"5th St Gym" ambayo ipo nchini marekani ni Gym kongwe na yenye heshima kubwa sana kwenye ulimwengu wa boxing kwani mabondia wengi wakubwa walishawahi kufanya mazoezi hapa kwenye hii Gym mfano, Muhammad Ali, David Haye, Benard Hopkins, Davin Haney, Roberto Duran na wengine wengi sana.
