Moja kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikivuruga mahusiano na kuharibu msingi wa imani kwenye ndoa au uchumba ni suala la kuchepuka (kusalitiana kwenye mapenzi).
Siku ya leo nchini Nigeria kuna picha inayosambaa mtandaoni ikionesha mwanamke ambaye anaonekana kupitia picha zilizonaswa na camera (CCTV) akiruka wigo wa nyumba kwa kutumia ngazi ikiwa ni nyakati za usiku na kutokana na chanzo cha taarifa hii inasemekana mwanamke huyo alikua akiruka ukuta huo aweze kwenda kwenye harakati zake za uchepukaji.
Ingekua wewe ni muhusika wa mahusiano hayo ni kipi ungekifanya?
