Taarifa iliyotufikia usiku huu inaeleza kuwa
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini Tanzania ambazo zitaanza kutumika kuanzia Jumatano June 01,2022.
Bei hizo za mafuta zimeshuka kutokana na ruzuku ya Tsh. Bilioni 100 ambayo Rais Samia aliagiza itolewe ili kuleta ahueni kwa Wananchi.
Kwa Dar es salaam bei ya Petroli baada ya ruzuku hii sasa itakuwa ni Tsh. 2994 badala ya Tsh. 3301 iliyokuwepo huku bei ya Dieseli ikiwa Tsh. 3131 badala ya Tsh. 3452.
EWURA imesema kushuka kwa bei za mafuta nchini kumechangiwa na ruzuku ya Tsh. Bilioni 100 ambayo Rais Samia aliagiza itolewe ambayo imesababisha kwa Bandari ya Dar es salaam petroli ishuke kwa Tsh. 306 kwa lita na dizeli imeshuka kwa Tsh. 320 kwa lita.
Bandari ya Tanga petroli imeshuka kwa Tsh. 152 kwa lita na dizeli kwa Tsh. 486 kwa lita na Bandari ya Mtwara petroli imeshuka kwa Tsh. 282 kwa lita na dizeli kwa Tsh. 486 kwa lita.
"Wauzaji wa Petroli wa rejareja na jumla watatakiwa kuuza mafuta kwa kutumia bei yenye ruzuku yeyote atakayekiuka agizo atachukuliwa hatua kali" Taaifa ya Ewura.
