Mmoja wa watu wa familia tajiri zaidi za kifalme duniani, Rais wa Sheikh Khalifa bin Zayed al-Nahyan wa Milki za kiarabu (UAE) amefariki akiwa na umri wa miaka 73.
Sheikh Khalifa alikuwa rais wa Milki za Kiarabu (UAE) tangu mwaka 2004, lakini wadhifa wake kwa kiasi kikubwa haukuwa na mamlaka tangu alipopata maradhi ya kiharusi mwaka 2014.
Kaka yake, Mohamed bin Zayed al-Nahyan, sasa ndiye anayeongoza masuala ya kitaifa.
Familia ya al-Nahyan inaaminiwa kuwa na utajiri wa thamani ya dola bilioni 150(£123bn).
Pamoja na kuwa Rais wa UAE, Sheikh Khalifa alikuwa mtawala wa Abu Dhabi, mji mkuu wenye utajiri wa mafuta wa milki saba zinazounda Muungano wa nchi za kiarabu
Taarifa ya kifo chake ilitangazwa katika Shirika rasmi la habari la WAM.
Wizara ya masuala ya rais ilitangaza siku 40 za maombolezo na kuperurushwa kwa bendera nusu mlingotikuanzia Ijumaa, na kazi zimeahirishwa katika sekta za umma na za kibinafsikwa muda wa siku tatu.
Sheikh Khalifa alichukua mamlaka kama rais wa pili wa UAE mwezi Novemba 2004 , akimrithi baba yake kama mtawala wa 16 wa Abu Dhabi.
