Taarifa ya kutoka Mkoani Mara inaeleza kuwa Jeshi la Polisi Mkoani Mara linamshikilia Gimusi Murimi (42), Mkazi wa Wilaya ya Serengeti kwa madai ya kumjeruhi mkewe kwa kumuingizia panga sehemu za siri akimtuhumu kuchepuka
Kamanda wa Polisi Mara, Longinus Tibishubwamu amesema Mtuhumiwa anafanya kazi Katoro, Geita na Mei 25, 2022 aliporejea nyumbani alibaini mkewe sio mwaminifu kwenye ndoa
Kamanda anasema "Akamshambulia kwa fimbo na baadaye kumwingizia panga sehemu za siri na
kumuumiza sana. Mwathirika yupo hospitali akipatiwa matibabu, uchunguzi unaendelea huku mtuhumiwa tukiwa tumemshikilia."
Credit to @serengetimediacentre
