
Uongozi wa kata ya Tandala wilaya ya Makete mkoani Njombe kupitia kikao cha kamati ya maendeleo ya kata umepitisha sheria ndogo ya kuwakamata wanawake watakaovaa nguo fupi pamoja na milegezo kwa wanaume na kuwatoza faini ya mifuko mitano ya saruji kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya msingi.