Mwili wa Vivian Richard Urasa (29) aliyeuawa na kutupwa kwenye shimo mbali kidogo na makazi ya Watu Makulu Jijini Dodoma umeagwa katika Kanisa la KKKT Cathedral tayari kwa kusafirishwa kuelekea Machame Moshi kwa mazishi.Akizungumza na AyoTV, Kamanda wa Polisi Dodoma Martine Otieno amethibitisha tukio hilo la mauaji na kusema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa chanzo cha kifo chake.“Tunaendelea na ufuatiliaji wa tukio hili, ni kweli Vivian Richard Urasa alikutwa ameuawa mwili ulionekana kama alivunjwa shingo na upande wake wa uso kama una majeraha, inaonekana ameuawa na Watu wasiojulikana”“Tunaendelea na uchunguzi na mpaka sasa tuna Mtu mmoja anayetiliwa mashaka ajulikanaye kwa jina la David, bado tunaendelea na mahojiano na kufuatilia vyanzo vingine ili kuhakikisha tunawatia mbaroni hawa Watu waliohusika na tukio hili”
Tags
bongo habari
