Mfanyabiashara wa Marekani Bill Gates yuko nchini Kenya na anatarajiwa kufanya msururu wa mazungumzo na Wakenya
Mwanzilishi huyo wa Microsoft anatazamiwa kukutana na maafisa wa serikali na washikadau wengine katika sekta ya kibinafsi.
Gates atazuru kaunti ya Makueni ambapo mwenyeji wake atakuwa Gavana Mutula Kilonzo Jnr.
Ripoti zinaonyesha kuwa atatembelea hospitali ya Mama na Mtoto ya Makueni na Kituo cha Afya cha Kathonzweni.
Pia atatembelea viongozi wa kitaifa na mitaa, washirika, na wafadhili na pia kukutana na wanasayansi wa kikanda na wavumbuzi.
Gates atatangaza kujitolea kwa Wakfu wa Bill & Melinda Gates Foundation kuunga mkono ubunifu na unaolenga kuboresha afya, usalama wa chakula, na usawa wa kijinsia katika nchi za Afrika.
