Lennon aliitwa kwa mara ya kwanza na kocha Sven-Goran Eriksson kwenye kikosi cha England kilichoshiriki michuano ya mwaka 2006 huko Ujerumani akiwa na miaka 19, akachezea England mchezo wake wa kwanza dhidi ya Trinidad and Tobago.

Ruka Twitter ujumbe, 2
Maelezo ya video,Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa Twitter ujumbe, 2

4. Sitastaafu baada ya fainali za Qatar - Bale

world cup

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Nahodha wa Wales, Gareth Bale amesema hafikirii kuachana na soka hata baada ya fainali za kombe la dunia huko Qatar zinazoanza Novemba 20, 2022.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 33, atakuwa na miaka 37 itakapofanyika fainali zingine, kama aliyonayo Christiano Ronaldo sasa anaye anakwenda kuiwakilisha Ureno huko Qatar.

Wales imeondoka leo, huku timu ya taifa ya mchezo wa Raga ikijipanga na kuwapigia makofi wachezaji hao wakiongozwa na Bale walipokuwa wanaondoka kwenda Qatar.

Ruka Twitter ujumbe, 3
Maelezo ya video,Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa Twitter ujumbe, 3

5. Ronaldo na Bruno Fernandes wasalimiana 'kitata'

Kiungo wa ortugal Joao Mario anasema kusalimiana kwa kupeana mkono kwa mashaka na kutazamana isivyo kawaida kati ya Cristiano Ronaldo na Bruno Fernandes siku ya Jumatatu, ilikuwa mzaha na "imetafsiriwa vibaya."

Kufuatia mahojiano ya Ronaldo na TalkTV, ambapo alisema alihisi "amesalitiwa" na Manchester United, sasa wengi walitaka kuona wachezaji hao wanaocheza pamoja United wakikutana watasalimianaje.

Salaam yao imeibua mjadala, kama Bruno kuonekana kutomtilia maanani Ronaldo, kama video inavyoonyesha.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya leo, Mario alisema: "Nilikuwa pale na niliona kila kitu, ilikuwa wakati wa kutaniana ambao ulitafsiriwa vibaya kwa nje.

Ruka Twitter ujumbe, 4
Maelezo ya video,

Mwisho wa Twitter ujumbe, 4