Kikosi cha Timu ya Taifa ya Ufaransa katika Kombe la Dunia 2022 kimekumbwa na ugonjwa siku moja kabla ya mechi yao muhimu ya Nusu Fainali dhidi ya Morocco.
Ugonjwa huo unaokuja na homa na kuumwa koo umeanza kusambaa kati ya wachezaji wa timu hiyo na kuleta wasiwasi mkubwa.
Dayot Upamecano alianza kujisikia vibaya, hivyo Jumatatu hakuweza kufika mazoezini. Kufikia Jumanne, Upamecano na Adrien Rabiot walikosa mazoezi sababu ya kuugua. Hali hii imelazimu kufanyika kwa maandalizi ya mabadiliko kwenye dakika za mwisho.
Hivi sasa, Ibrahima Konate na Youssef Fofana wako wameandaliwa ikiwa Dayot na Adrien watashindwa kucheza.
Tetesi zinasema kuwa Karim Benzema ambaye amekuwa majeruhi na kushindwa kucheza hata mechi moja ya Kombe hili la Dunia,sasa yupo fit na ameshaanza mazoezi tangu Jumamosi, hivyo atakuwa tayari kujumuika na kikosi ikiwa atahitajika.
Toa maoni yako
#Sports
#M31