Klabu ya Simba ya Tanzania, imepangwa katika Group C katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, ambapo itakutana na Vipers kutoka Uganda, Horoya ya Guinea na Raja Cassablanca ya Morocco.
SImba ilifanikiwa kuingia katika Hatua ya Makundi katika mashindano ya Klabu Bingwa na sasa itakuwa na kazi ya kupambana na miamba hiyo, ili kusonga mbele.
Ikumbukwe kwamba Raja Cassablanca, inatokea Morocco na baadhi ya wachezaji wake, wapo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kinachoendelea kuwashangaza wengi katika mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Qatar ambapo wameingia hatua ya nusu fainali.
