Ni wazi kwamba kwenye soko la simu janja za kukunja na kukunjua Kampuni ya Samsung kupitia simu zao za Samsung Galaxy Z Fold 4 Na Samsung Galaxy Flip 4 ndio wameshikilia usukani.
Vipi kuhusiana na makampuni mengine? Ni wazi kuwa yameingia katika aina hii ya simu janja lakini ni kwamba bado ushindani ni mkubwa sana kwa wakongwe hao, Samsung.
Kampuni ya Oppo hivi karibuni ilitoa toleo lake la pili katika muendelezo wa Oppo Find N2 Flip na toleo hili ni moja kati ya washindani wazuri wa matoleo ya aina hiyo.
Kwa toleo hili kutoka Oppo wengi wanadai kwamba pengine hili ndio toleo sahihi la kushindanishia simu za aina hii kutoka Samsmung.
Kwa sasa kuna baadhi ya picha zinasambaa mtandaoni zikidai kuwa ndio toleo la Galaxy Z Flip 5 likiwa na kioo kikubwa zaidi ukilinganisha na toleo lililopita.
Kingine ni kwamba kama kioo cha nje cha Oppo Find N2 Flip Kilikushtua basi cha Galaxy Z Flip 5 kitakushtua zaidi maana ni kikubwa kuliko hicho.
Kupitia chanzo cha Ice Universe ambao mara nyingi huwa wanaweka wazi mambo ya Samsung kabla ya wakati na mara nyingi mambo hayo yanakuaga sahihi ndio wamekuja na hii fununu.
Mambo mengine kama vile sifa za undani, hayajawekwa wazi kwa sasa na kampuni, hii ni mpaka kampuni yenyewe ikifanya uzinduzi kama kawaida.