Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Corona .
Samia amewaongoza maafisa wengine wa serikali wakiwemo Waziri mkuu Kassim Majaaliwa kupokea chanjo hiyo .
Katika uzinduzi wa hafla ya chanjo chini humo rais Samia amesema serikali yake itahakikisha kwamba kila mtanzania nayetaka kuchanjwa anapata chanjo hiyo .
‘Mimi ni mama ya watoto wanne,mimi ni bibi wa wajukuu kadhaa na pia mimi ni mke ..siwezi kujiweka katika hatari … Nimekubali kwa hiyari yangu na najua ndani ya mwili wangu nina chanjo kadhaa na nimeishi nazo kwa miaka karibu 61’ alisema rais Samia kabla ya kuchanjwa.
Katika hotba yake wakati wa uzinduzi huo rais Samia aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo akisema kuna walioathiriwa na kuwapoteza jamaa zao ambao wangefurahia kuipata chanjo hiyo mapema .
‘ Wakati gonjwa hili linapokuguza ndipo utajua hatari yake…nenda Moshi,nenda Kagera ,nenda Arusha..wana maneno ya kukuambia’ alisema rais Samia .
Rais Samia alisema kuna Watanzania ambao tayari walishachanjwa nje ya nchi ili kuendelea na shughuli zao za kibiashara na kikazi .
‘Tunajua watu ambao wameshanjwa.Wameeda kuchanja Afrika Kusini au Dubai ..na wanajua kama hawangechanjwa wangezuilika kufanya biashara huko’
Aliongeza kuwa kuna makundi ya watu ndani ya nchi hiyo waliotaka kuruhusiwa kuleta chanjo hapo awali .
Jumuiya ya Wachina ilitaka kukubaliwa kuleta chanjo yao lakini serikali wakati huo ilikataa ila baadaye walikubaliwa na wamechanja .
Samia pia aliongeza kwamba wafanyikazi wa taasisi za kimataifa pia sasa wameruhusiswa kuleta chanjo na wanaendelea kuchanjwa .
Dozi Zaidi
Rais Samia amesema Tanzania imeagiza dozi zaidi za chanjo ya Johnson and Johnson kupitia Umoja wa Afrika kama alivyoshauriwa na mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na kuzuia magonjwa barani Afrika (Africa CDC) Dkt. John Nkengasong, wakati alipofanya mazungumzo naye siku ya jumanne .
‘Kwa walio tayari kuchanjwa tutahakikisha wanaipata ..chanjo ni imani . Mimi nimechanjwa mara tano au sita,’ alisema rais Samia
Chanjo katika Mikoa
Serikali kupitia wizara ya Afya nchini humo imesema dozi za chanjo zitapelekwa katika kila mkoa wa taifa hilo ili kuhakikisha kwambawatu wanachanjwa.
Mkurugenzi wa Kinga Leonard Subi amesema wameamua kupeleka chanjo katika kila mkoa ili kutowabagua wanaotaka kuchanjwa kinyume na mpango wa hapo awali wa kuipeleka chanjo katika mikoakumi mikubwa.
Chanjo hiyo itatolewa kwa usawa kulingana na idadi ya watu na mahitaji yake Waziri wa Afya Dorothy Gwajima amesema jana kwamba chanjo zitakazotumiwa pole pole katika maeneo mengine zitahamishwa hadi katika sehemu zinazowachanja watu kwa haraka.
Bi.Gwajima amesema mpango wa chanjo utawalenga watu katika makundi ya vipaumbele kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali.
Aliongeza kwamba chanjo nyingine zinatarajiwa nchini wanapoendelea kuzitumia zaidi ya dozi milioni moja zilizongia Tanzania mwisho mwa wiki kupitia mpango wa Covax.