Tanzania yazindua utoaji wa chanjo
Tanzania leo inazindua zoezi lake la utoaji chanjo ya Corona katika hafla ambayo rais Samia Suluhu anatarajiwa kuchanjwa katika Ikulu ya Dar es Salaam.
Serikali kupitia wizara ya Afya nchini humo imesema dozi za chanjo zitapelekwa katika kila mkoa wa taifa hilo ili kuhakikisha kwambawatu wanachanjwa.
Mkurugenzi wa Kinga Leonard Subi amesema wameamua kupeleka chanjo katika kila mkoa ili kutowabagua wanaotaka kuchanjwa kinyume na mpango wa hapo awali wa kuipeleka chanjo katika mikoakumi mikubwa .
Chanjo hiyo itatolewa kwa usawa kulingana na idadi ya watu na mahitaji yake Waziri wa Afya Dorothy Gwajima amesema jana kwamba chanjo zitakazotumiwa pole pole katika maeneo mengine zitahamishwa hadi katika sehemu zinazowachanja watu kwa haraka .
Bi.Gwajima amesema mpango wa chanjo utawalenga watu katika makundi ya vipaumbele kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali.
Aliongeza kwamba chanjo nyingine zinatarajiwa nchini wanapoendelea kuzitumia zaidi ya dozi milioni moja zilizongia Tanzania mwisho mwa wiki kupitia mpango wa Covax.