Tetesi za soka Ulaya: Man united inamtaka 'mzee' Sergio Ramos

 

Tetesi za soka Ulaya: Man united inamtaka 'mzee' Sergio Ramos



Manchester United wanatafuta kuimarisha safu ya ulinzi huku beki mkongwe wa zamani wa Real Madrid, Sergio Ramos, 39, akitajwa kama chaguo baada ya kuondoka kwenye klaby yake ya Monterrey ya Mexico. (Fichajes)

Roma wameanza mazungumzo rasmi ya kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 24, kutoka Manchester United kwa mkopo wenye wajibu wa kumnunua kwa £30m. (Gazzetta dello Sport)

West Ham wamekuwa wakimfuatilia mshambuliaji wa Rio Ave, Clayton mwenye umri wa miaka 26, raia wa Brazil, ambaye ni miongoni mwa wafungaji kinara wa Ligi Kuu ya Ureno. (Teamtalk)

Kiungo wa zamani wa Arsenal Matteo Guendouzi, 26, anayekipiga Lazio, anasakwa na Sunderland, ambao wamewasilisha ofa ya £21.4m. (Sunderland Echo)

Beki wa Ufaransa Ibrahima Konate, 26, anaingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake msimu ujao, lakini bado anaweza kusaini mkataba mpya na Liverpool katika wiki zijazo. (Football Inside

Kiungo wa zamani wa England na Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 32, anataka kurejea ligi kuu England (EPL) mwezi Januari baada ya kuwa mchezaji huru tangu alipoondoka Besiktas mwezi Agosti. (The Athletic)

Mshambuliaji wa England Ivan Toney, 29, haitarajiwi kuondoka Al-Ahli mwezi Januari kurejea EPL kutokana na sababu za kodi. (Talksport)


West Ham wamepata pigo katika jitihada za kumsajili Promise David wa Union Saint-Gilloise, kwani mchezaji huyo wa Canada, 24, hataki kuachana na Ligi ya Mabingwa na kujiunga na timu inayopambana kutoshuka daraja. (Talksport)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post