Serikali imesema itatatua changamoto ya vifaa katika Sekta ya Filamu kwa kuanzisha maktaba itakayokuwa na vifaa vya aina mbalimbali viyakavyotumika katika Tasnia hiyo.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa alipokutana na Waigizaji wa Tamthilia ya Tunu katika Hospitali ya Kairuki DSM.
"Serikali na Watanzania tupo pamoja na nyinyi na tunawakubali sana Waigizaji wetu na vipaji mlivyonavyo, tumejipanga kuwasaidia kutengeneza Filamu bora ili Watanzania wanaoutuunga mkono waendelee kuburudika kwa Filamu nzuri”- BASHUNGWA
"Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha ajira Milioni 800 ambazo tumeahidi kwenye Ilani ya CCM, Tasnia ya Sanaa na Michezo tutatoa mchango mkubwa na tutafanya hivi kwa kushughulika kwa changamoto ambazo mnakabiliana nazo ikiwemo vifaa ambapo tuna mpango wa kujenga maktaba ya vifaa ili Maproducer, Waigizaji wawe wanachukua kwa utaratibu kama ilivyo Maktaba za Vitabu”- BASHUNGWA
#MillardAyoUPDATES