RAISU MUSEVEN:SITAKI VITA

0

 

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema amesikitishwa na kitendo cha mahindi ya Uganda kuzuiwa kuingizwa kwenye baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki na kusema hiyo sio ishara nzuri kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki huku akisema Uganda haitolipiza kisasi bali itatumia njia nzuri ya mazungumzo ili kulinda Umoja wa Afrika Mashariki.
“Nilisikia kuna baadhi ya Wabunge wanazungumza kuhusu kulipiza kisasi (kwenye ishu ya mahindi ya Uganda kuzuiliwa kwenye baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki), siungi mkono visasi, tuwe wavumilivu na tulimalize hili vizuri kwa maslahi mapana ya Jumuiya ya Afrika Mashariki”-MUSEVENI
“Kwakuwa Afrika Mashariki ina Nchi tofauti wale Wazee wa Fursa na Wanyonyaji lazima tu watakuwepo, kuna Wanyonyaji kwenye baadhi ya Nchi wanasema mahindi ya Uganda yatavuruga biashara zao, tunahitaji mazungumzo, muingiliano na ushirikiano sio tu kupiga kelele tupu”- MUSEVENI
#MillardAyoUPDATES

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable