Mahakama ya Maryland Marekani imemuhukumu kifungo cha mwaka mmoja Rubani wa zamani wa Shirika la Ndege la Southwest la Nchini humo na kumpiga faini ya $5,000 (Tsh. milioni 11.5) kwa kosa la kutazama video ya ngono akiwa kazini kwenye chumba cha Marubani huku Ndege ikiwa angani.
Rubahi huyo Michael Haak mwenye umri wa miaka 60 siku ya tukio anadaiwa kutoa nguo mbele ya Rubani mwenzake ambae alikua Mwanamke ndani ya chumba cha Marubani huku akitazama video hiyo kwenye Ndege hiyo iliyokua inaruka kutoka Philadelphia kuelekea Orlando Agosti 10 mwaka 2020.
Haak alikuwa Rubani wa Southwest kwa miaka 27 kabla ya kustaafu mwishoni wa Agosti 2020 ambapo hata hivyo kitendo hicho kimempa hasara ya kusitishiwa mafao yake kutoka kwenye Shirika hilo la Ndege ikiwa ni adhabu kwa kuhatarisha maisha ya abiria na kuchafua jina la Southwest.
