"NAVUTIWA SANA NA RICH MAVOKO"-FID Q

0

 


Rapper @therealfidq 'FidQ' amemtaja Rich Mavoko kama ni miongoni mwa wasanii wanne anaovutiwa nao kutokana na ufanisi alionao katika kazi yake ya sanaa.

Licha ya kutoweka wazi wasanii wengine anao wakubali Mzee Mbuzi huyo ameandika “kuna huyu @richmavoko halafu kuna wengine kama watatu au wanne, ninavutiwa sana na Tungo zao pamoja na ufanisi wa mawimbi ya sauti wanaouweka kwenye uimbaji wao”.
Huku akimuongeza Rapper @aytanzania Masta na wasanii wengine waliobaki akisema wamuache kwanza.
Fid ameweka wazi mahaba yake ikiwa ni siku mbili tu tangu zipite baada ya kuachia ngoma yake mpya ‘Mapenzi’ ambayo inaendelea kufanya poa huko YouTube ikiwa nafasi ya 11 On Trending For Music huku ikiwa na views zaidi ya Milioni 1, huku miaka mitatu iliyopita wawili hao walikutana kwenye wimbo mmoja unaitwa ‘Sheri’.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable