Bendera ya Hamas kupigwa marufuku Ujerumani


Vyama vya Umoja wa Kikristo (CDU / CSU) na vikundi vya Bundestag vya Social Democratic Party (SPD), ambavyo viliunda serikali ya muungano nchini Ujerumani, vilikubaliana kupiga marufuku bendera ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas).

Kulingana na taarifa katika gazeti la Welt, CDU / CSU na SPD zinalenga kupiga marufuku bendera ya Hamas kwa kuongeza kwenye Ibara ya 86 ya Kanuni ya Adhabu ya Ujerumani, ambayo inadhibiti marufuku ya propaganda dhidi ya vyombo visivyo vya katiba.

Katika taarifa ya gazeti juu ya mada hiyo, Naibu Mwenyekiti wa chama cha Umoja wa Vyama vya Muungano Thorsten Frei alisema:

"Hatutaki kuruhusu bendera za mashirika ya kigaidi kupepea kwenye ardhi ya Ujerumani,"

Thorsten Frei pia alisema kuwa kwa marufuku hayo, watakuwa wakitoa ujumbe wazi wa msaada kwa raia wa Kiyahudi wanaoishi nchini humo.

Ombi la kanuni linatarajiwa kutumwa kwa Bunge Kuu la Bundestag wiki ijayo.

Jumuiya ya Ulaya ilijumuisha Hamas kwenye orodha ya "mashirika ya kigaidi" mnamo mwaka 2001.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post