Na Juma Mizungu, Pwani
Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kibaha Vijijini na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kutokea Wilaya ya Kibaha Vijijini na Mdau wa maendeleo Wilaya ya Kibaha Vijijini Mhe. Hamoud Abuu Jumaa amechangia mchango wa shilingi milioni mbili kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Secondari ya Kawawa.
Mhe. Hamoud Abuu Jumaa amefanya hivyo baada ya kupokea barua ya mwaliko ya kushiriki katika zoezi la kuchangia Ujenzi wa kupauwa madarasa matatu kwa ajili Shule ya Secondari ya Kawawa. Zoezi hilo limekuja baada ya ongezeko la ufaulu kwa watoto wengi ambao wamejiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021.
Mhe. Hamoud Abuu ameleza kwamba mchango huo wa shilingi milioni mbili ni fedha zilizo toka kwa marafiki zake wawili ambao wameguswa na Ujenzi wa Shule hiyo ambayo itasaidia Watoto wengi kupata Elimu ya Secondari katika maeneo yao.
Mhe. Hamoud Abuu Jumaa amewashukuru marafiki zake wawili ambao ni Mhe. William Tate Ole Nasha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Uwekezaji) pamoja na Mbunge wa Kibaha Mjini Mhe. Silvestry Fransic Koka ambao wote walichangia kiasi cha shilingi milioni moja kila mmoja.
Mhe. Hamoud alimalizia kwa kusema bado michango inaendelea kutoka kwa marafiki zake wengine ambao wamemuahidi kumchangia ili kufanikisha Ujenzi wa Secondari hiyo mpya katika Kata ya Kawawa lakini pia ameahidi kuendelea kushirikiana na Viongozi wa Kata ya Janga ili kufanikisha jambo hilo.