Christian Erikson: Jinsi kifaa hiki atakachoweka mchezaji huyo kinavyofanya kazi

Eriksen alihitaji matibabu ya dharura kabla ya kukimbizwa hopsitalini

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Eriksen alihitaji matibabu ya dharura kabla ya kukimbizwa hopsitalini

Moyo wa mchezaji wa Denmark Christian Eriksen uliwacha kupiga kwa muda wakati wa mechi ya kombe la Euro wiki iliopita.

Eriksen alilazwa hospitalini kwa dharura ambapo alithibitishwa kwamba hali yake ni shwari katika mazingira aliokuwa.

Madaktari walithibitisha kwamba Eriksen mwenye umri wa miaka 29 alipata mshtuko wa moyo na kuamua kwamba atawekewa kifaa kitakachokuwa kikisaidia moyo kupiga.

Hatua hiyo ni muhimu kutokana na usumbufu unaotokana na moyo kukosa kusukuma damu inavyohitajika , kama inavyoelezewa na daktari wa timu ya Denmark Morten Boesen.

Je kifaa hicho kinachowekwa mwilini kinafanya kazi vipi?

Kifaa hicho kinachopandikizwa mwilini kwa jina cardioverter defibrillator , ni betri ndogo inayovaliwa kifuani kuchunguza jinsi moyo unavyosukuma damu ili kubaini iwapo moyo hausukumi damu unavyohitajika.

Defibrillator ya aina hiyo hutoa msukumo wa umeme kupitia waya moja ama zaidi zilizounganishwa na moyo , ili kurekebisha mapigo ya moyo yasio ya kawaida , ilielezea kliniki ya Mayo katika tovuti yake `nchini Marekani.

Wagonjwa wanaohitaji kifaa hicho ni kwasababu mapigo ya moyo yao ni ya haraka ama wanakabiliwa na mapigo yasio ya kawaida hali inayozuia moyo kusukuma damu ya kutosha katika maeneo mengine ya mwili.

Mbali na kuusaidia moyo kuendelea kusukuma damu pia huchunguza moyo na kuupa `nguvu unapohitaji kusukuma damu .

Inafaa kujulikana kwamba kifaa hicho cha Defibrillator sio sawa na pacemaker , kifaa chengine kinachopandikizwa mwilini ili kusaidia kuthibiti mapigo ya moyo yasio ya kawaida.

''Christian alikubali suluhu hiyo na pia mpango huo ulithibitishwa na wataalam kitaifa na kimataifa ambao walipendekeza apatiwe tiba hiyo'', aliongezera Dkt Boesen.

Eriksen- mchezaji wa zamani wa Tottenham Hotspurs ambaye kwa sasa anaichezea Inter Milan , alianguka na kuzirai muda mfupi kabla ya kipidi cha mapumziko katika mechi kati ya Denmark na Finland na alilazimika kufufuliwa na kifaa cha defibrillator.

Mashujaa waliomuokoa mchezaji wa Denmark Christian Eriksen

Daktari wa Ujerumani Jens Kleinfiled , aliyemtibu uwanjani , aliambia chombo cha habari cha Funkie kwamba" takriban sekunde 30 baadaye alifungua macho na nikaweza kuzungumza naye.."

"Ulikuwa ni wakati uliojawa na hisia , kwasababu katika dharura kama hizo katika maisha ya kila siku fursa ya mtu kupona ni chache'', aliongezea.

Eriksen akiwa hospitali

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Kleinefeld alisema kwamba wakati huo alimuuliza Eriksen , je umerudi kwetu?''

"Ndio nimerudi niko nanyi tena'', alijibu Eriksen . Nina miaka 29 pekee."

"Ni wakati huo ndiposa nikagundua kwamba ubongo wake haukuharibika," alisema Dr. Kleinefeld.

Tukio kama hilo

Beki wa Ajax na Uholanzi Daley Blind pia alikutwa na tatizo la moyo mwezi Disemba 2019.

Lakini hatua hiyo haikumlazimu kuwacha uchezaji wake wa kulipwa na alirudi uwanjani mwezi Februari 2020 baada ya kupandikizwa mwilini kifaa cha defibrillator.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi katika michuano ya Euro 2020 na alishiriki katika mechi yake ya kwanza, ambayo iliishia 3-2 dhidi ya Ukraine.

Hatahivyo, mchezaji wa mpira wa kriketi James Taylor alimaliza uchezaji wake na tatizo la moyo 2016.

Mwanakriketi James Taylor

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Alilazimika kupandikizwa kifaa cha Defibrillator na kuambia BBC Sport kile ambacho Eriksen anatarajia.

''Ni defibrillator kilichopo ndani yangu'' , Taylor alielezea.

Kile ninachoweza kuelezea ni kwamba ni nusu ya simu ya kawaida na ni kizito kiasi. Kina nyaya mbili ambazo zimeunganishwa chini ya moyo.

"Mara ya kwanza nilikuwa na wasiwasi kuwekwa kifaa hicho lakini baada ya kuelewa kuhusu hali yangu na jinsi kitakavyonisaidia , kimekuwa rafiki yangu mkubwa'' , alisema.

''Niliamua kukiweka katika misuli yangu ya kifuani , hivyobasi siwezi kukiona, lakini unaweza kuona waya kifuani mwangu, ukitaka'', alisema.

Kitu muhimu , naweza kusema ni kuzungumza na watu unaowaamini na pia kuzungumza na watu ambao wamekuwa na uzoefu kama huo ili kujifunza na kuelewa hali , kwasababu hakuna anayejua zaidi'', alisema.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post