Faida ya kutumia juisi ya karoti


Mchanganyiko huo pia hutumika kama kinga dhidi ya saratani, matumizi ya juisi ya karoti yenye mchanganyiko wa tangawizi husaidia kuukinga mwili dhidi ya matatizo ya saratani za aina mbalimbali kwani husaidia kuua seli zinazoweza kuchangia matatizo ya saratani.

Hulinda meno na fizi, karoti pekee yake kwanza inatosha kwa kuwa mlinzi mzuri wa kinywa, hivyo matumizi ya glasi moja ya juisi ya karoti iliyochanganywa na tangawizi baada ya kula husaidia pia kulinda afya ya kinywa kwa ujumla.

Matumizi ya juisi ya karoti nayo husaidia kuimarisha kinga za mwili na kumlinda mhusika dhidi ya magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya macho, kutokana na karoti kuwa na vitamin A ya kutosha.

Juisi hiyo ya karoti inasifika kwa kuimarisha mifupa, kutokana na kuwa na madini ya ‘potassium’ ambayo hupatikana ndani yake.

Sambamba na hayo, mchanganyiko wa matunda ya aina tatu yaani matikitimaji, tufaa (apple) pamoja na karoti ambavyo huweza kujenga na kuimarisha kinga za mwili endapo yataandaliwa vizuri.

Matunda hayo kwa pamoja yatahitajika kuandaliwa vizuri kwa kuyaosha na kutoa maganda pamoja na mbegu na kisha kuchanganywa kwa pamoja na baadaye kusagwa, huku ukianza na tufaa na matikitimaji na baadaye kuchanganywa kwa pamoja na karoti iliyosagwa .

Baada ya mchanganyiko huo kusagika unashauriwa kuchuja mara moja na kuweka kwenye jagi na baadaye kuongeza kiwango kidogo sana cha sukari au kutoweka kabisa, kisha utatumia mchanganyiko huo kunywa asubuhi na jioni kila siku kikombe kimoja . Fanya zoezi hilo angalau kwa miezi miwili mfululizo na itakusaidia katika kukukinga dhidi ya magonjwa ya mara kwa mara.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post