Maaskofu nchini Marekani wana uwezekano wa kuwa na mgongano na haja ya Bw Joe Biden baada ya kupiga kura ya kuidhinisha waraka ambao unaweza kutaka azuiwe kupokea Sakramenti ya Ushirika Mtakatifu( Ekaristi Takatifu)
Mkutano Mkuu wa maaskofu wa Katoliki nchini Marekani (USCCB) ulibishana kwenye mtandao juu ya iwapo utaandaa waraka wa mafunzo juu ya wanasiasa wanaounga mkono utoaji mimba.
Ushirika Mtakatifu ni ibada muhimu katika imani ya mkristo Mkatoliki.
Rais Biden ambaye ni Mkatoliki huhudhuria ibada mara kwa mara.
Akijibu kuhusu kura iliyopigwa na maaskofu, Bw Biden alisema : "hayo ni mambo ya kibinafsi na sidhani kama itatokea ."
Vatcan tayari imeashiria kupinga hatua ya maaskofu wa Marekani.
Baada ya mjadala wao Alhamisi , Askofu Allen H Vigneron, makamu-rais wa USCCB, alitangaza kuwa hatua hiyo ilipitishwa na maaskofu 168 kwa 55 waliopinga, na sita hawakuwepo.
Maaskofu wa Marekani wamegawanyika pakubwa juu ya suala la otoaaji mimba. Askofu Mkuu wa San Diego Robert McElroy, alionya kuwa waraka wa aina hiyo unaweza kusababisha "kutumiwa kama silaha " kwa Ekaristi takatifu (jina linalotumiwa zaidi kwa Ushirika mtakatifu ).
Hatahivyo, Liam Cary, Askofu wa Baker, Oregon, amesema kuwa kanisa liko katika "hali isiyo kuwa ya kawaida", likiwa na " Rais Mkatoliki ambaye anapinga mafundisho " ya Kanisa.
Wito wa Vatican
Waraka huo hautaandikwa na kamati ya mafundisho ya kikatoliki ya maaskofu wa Marekani
Hatahivyo, ingawa itakuwa ni muundo wa sera ya taifa, haitakuwa lazima kufuatwa. Kila askofu binafsi ana haki ya kuamua ni nani anayepaswa kuzuiw kushiriki misa (ibada) katika jimbo lake la kikatoliki.
Waraka huo utarudishwa kwa ajili ya kujadiliwa katika mkutano ujao wa Mkutano Mkuu wa maaskofu wa Katoliki wa Marekani mwezi Novemba.
Suala lenye utata juu ya iwapo wanasiasa wanaounga mkono utoaji mimba wanapaswa kushiriki ibad na kupokea Ekaristi limepata umaarufu zaidi wakati wa uchaguzi wa Bw Biden kama rais.
Kardinali Cupich, askofu mkuu wa Chicago, aliwaonya mapadri wengi kwamba ''angeshangaa sana kama atasikia maaskofu sasa wanataka kuongea kuhusu kuwatenga watu katika wakati ambapo changamoto halisi mbele yao ni kuwakaribisha watu tena kushiriki na kutekeleza imani yao na kujenga upya jamii zao ".
Hatahivyo, alipendekeza hoja hiyo, Askofu Kevin Roades, wa Fort Wayne-South Bend, alisema: "Tunawalenga watu fulani binafsi au suala moja, lakini ninadhani tunahitaji kukubali nidhamu ya kanisa kwamba wale wanaotenda dhambi kubwa hawapaswi kushiriki ushirika Mtakatifu ."
Kardinali Luis Ladaria - ambaye ni mkuu wa congamano la Mafundisho ya Imani, ambalo husimamia mafundisho ya kidini au theolojia ya Vatcan - aliutaka Mkutano Mkuu wa Maaskofu wa Katoliki wa Marekani kuchelewesha mjada huo.
Aliuandikia Mkutano huo akisema itakuwa ni "upotoshaji "kusema utoaji mimba na kuua mtu bila kumuumiza ndio "mambo mabaya zaidi katika maadili ya ukatoliki na mafundisho ya jamii ambayo yanahitaji uwajibikaji kamili kwa upande wa Wakatoliki ".
Catholics for Choice, ambacho kikundi cha haki ya kutoa mimba , kilisema kimesikitishwa sana na hatua ya maaskofu.
Katika taarifa yake, rais wa kikundi hicho , Jamie Manson, alisema: "Katika nchi na kanisa ambavyo vinakabiliwa na wasi wasi na mgawanyiko, leo maaskofu wameamua kuchagua upendelea badala ya uchungaji, ukatili kuliko kuwa kama Kristo."
Lakini alisema kuwa maaskofu wachache waliozungumza wazi dhidi ya hatua hiyo wanaleta mwangaza wa matumaini.
Joe Bidenni rais wa pili Mkatoliki kuchaguliwa nchini Marekani, baada ya John F Kennedy. Anaweza kuwa rais wa kwanza kunyimwa Ushirika Mtakatifu( Ekaristi Takatifu) na Kanisa -jambo litakalosisitiza mgawanyiko kuhusu utoaji mimba katika siasa za Marekani na maisha ya kidini