Nchini Morocco yanaitwa maeneo ya Morocco yaliyochukuliwa ya "Sebtah na Melilah". Lakini kwingineko duniani yanaitwa maeneo ya Uhispania ya Ceuta na Melilla yaliyoko Afrika Magharibi.
Ndio kipande pekee cha eneo la Ulaya kinachopatikana katika bara la Afrika-ukweli wa kisiasa na kisheria ambao haujawahi kutambuliwa na morocco, ambayo imeendelea kudai kurejeshwa kwake, pamoja na maeneo mengine matatu madogo katika bahari ya Mediterranean, yote yakiwa katika mlango bahari wa Gibraltar.
Mwezi uliopita, idadi kubwa ya wahamiaji walivuka mpaka kwa siku moja -8,000 kati yao wakiwa ni Wamorocco. Iligundulika kwamba walinzi wa Morocco walikuwa wamewaacha kwa makusudi wahamiaji wavuke.
Ghafla tukio hilo liligeuka na kuwa mzozo wa kidiplomasia baina ya Uhispania na Morocco, jambo lilililoifanya serikali ya Uhispania kutuma wanajeshi wake zaidi katika maeneo hayo na waziri mkuu Pedro Sanchez alielezea tukio hilo kuwa ''mzozo ambao haukutarajiwa uliowahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni baina ya Muungano wa Ulaya na Morocco ".
Wakati mzozo huo ukiendelea, Wamorocco walianza kampeni yao kwenye mtandao wa Twitter, yenye kauli mbiu inayosema : "Ceuta na Melilla sio Uhispania" na "Ceuta na Melilla ni maeneo ya Morocco - maliza ukoloni ''.
Vyombo vya habari viliripoti kuhusu matukio mabaya ndani ya eneo la Ceuta vikionesha makabiliano ya hasira baina ya Waandamanaji Wahispania wakikabiliana na wahamiaji na wanawake wa Kiislam wenye asili ya Morocco.
"Hawa sio wahamiaji, wako katika nchi yao," mtu mmoja alituma ujumbe wa Twitter.
'Ukoloni halisi wa Ulaya'
Ghafla ilionekana kwamba kushindwa kwa walinzi wa Morocco kuzuia kuingia kwa wahamiaji kwenye visiwa hivyo haikuwa ajali, bali lilikuwa ni jaribio la makusudi la kutuma ujumbe wa onyo kwa Uhispania kwa kumpokea Brahim Ghali, kiongozi wa Polisario Front, kikundi ambacho kinafanya kampeni ya uhuru wa eneo la Sahara Magharibi.
Uhispania , sawa na nchi nyingine nyingi, haijawahi kuyatambua madai ya Morocco ya eneo hilo, na mahakama ya Uhispania Jumanne ilikataa kutoa uamuazi juu ya mashitaka ya uhalifu wa kivita yanayomkabili Bw Ghali, ikisema kuwa kulikuwa na ukosefu wa ushahidi dhidi yake.
Lakini kuna maafikiano mengi katika Morocco kwamba sahara Magharibi ni ya Wamorocco kama ilivyo kwa Ceuta na Melilla.
Kwa mtazamo, madai ya Wamorocco juu ya eneo hilo yanaonekana kuwa sahihi.
Maeneo hayo ya miji yapo katika ardhi ya Afrika, huku Uhispania ikiwa Ulaya. Inaonekana kama ni ukoloni halisi wa Ulaya.
Historia fupi ya Ceuta na Melilla :
- Karne ya 15 : Melilla ilitawaliwa na Uhispania
- Karne ya 17 : Ceuta ilichukuliwa na kuwa chini ya utawala wa Uhispania
- Mwaka 1956: Uhispania ilibakia na Ceuta na Melilla baada ya Morocco kuwa huru
Ukumbusho wa 'udhalilishwaji ' wa Waislam
Vyanzo vya Waarabu vinaelezea eneo la Ceuta kama mwanzo wa juhudi za Waislam za kuitwa rasi ya Iberia katika karne ya 8, uvamizi ambao ulidumu kwa miaka 800.
Bandari hizo zilichukuliwa tena katika kile kilichofahamika kama Reconquista - harakati za kijeshi za kuwaondoa Waislam kutoka katika kile ambacho sasa kinafahamika kama Uhispani na Ureno.
Miji yote miwili ilitwaliwa na Uhispani baina ya karne ya 15 na karene ya 16 - karibu wakati sawa na wakati ambao Christopher Columbus alikuwa ana "gundua " Marekani na kutoa fursa hatimaye ya ukoloni wa Ulaya wa Amerika zote, kaskazini na Kusini.
Kwa Waislam, Ceuta na Melilla ni ukumbusho unaoumiza kushindwa na kudhalilishwa na mwamko wa magharibi, mamlaka za kikristo.
"Ni ardhi ya Waislam hata uvamizi udumu kwa muda gani , na jeraha la zamani ambalo baadhi wanafikiria limepona, lakini linaendelea kutiririka damuna hakuna tiba nyingine zaidi ya kulichukua tena eneo hilo ," ndivyo chapisho moja la Kiarabu lilivyoelezea hisia kuyahusu maeneo haya.
Hata mtandao wa kiarabu wa Wikipedia unaielezea miji hiyo miwili kama ya Morocco iliyo chini ya udhibiti wa Uhispania.
Hatahivyo, ingawa Morocco iliingia vitani kuchukua eneo la Sahara Magharibi baada ya Uhispania baada ya Uhispania kuondoka kwenye eneo hilo mwaka 1975, mwamko wa kurejesha tena udhibiti Ceuta na Melilla haujashabikiwa sana.
Morocco ilisindwa kuweka msukumo wa hoja yake katika Umoja wa Mataifa, uijumuishe miji hiyo katika eneo lake ambayo bado hayajaondolewa chini ya ukoloni, ambayo yanafahamika kama maeneo ambayo hayajajitawala.
Mwanasayansi wa Morocco Samir Bennis anasema baada ya uhuru kutoka kwa Uhispania na Ufaransa, Morocco ilitoa maeneo hayo kwa imani ikidhania kwamba suala litatatuliwa na baadaye, lakini Wahispania hawakujibu kwa ukarimu.
"Julai 6 1963, marehemu Mfalme King Hassan II [ wa Morocco] na Jenerali Franco [mtawala wa uhispania] walikutana katika uwanja wa ndege wa Barajas mjini Madrid kuzungumzia masuala yao ya mzozo wa mipaka.
Hadi leo, Uhispania imekataa kata kata mazungumzo ya aina yoyote kuhusu miji hii miwili, na kusisitiza kuwa imekuwa ya Uhispania kwa zaidi ya karne tano na kwamba ni sehemu ya jimbo la Uhispania.
Lakini baadhi wanajiuliza ni kwa misingi gani ya kihistoria na kisheria?