Kim Jong Un: Je kiongozi wa Korea Kaskazini anayeogopwa anaishi maisha gani?

Umaarufu wa Kim Jong Il umetokana zaidi na namna anavyozitisha nchi za magharibi na Marekani

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Umaarufu wa Kim Jong Il umetokana zaidi na namna anavyozitisha nchi za magharibi na Marekani

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon Un, ni mmoja wa viongozi wa dunia ambaye amekuwa na mvuto wa hali ya juu iwe kwa wanaompenda, wasio mpenda na hata wanaotaka kumfahamu zaidi tangu alipokuwa kiongozi wa nchi takriban muongo mmoja uliopita.

Umaarufu wake umetokana zaidi na namna ambavyo amekuwa tisho kwa nchi za magharibi hususan kutokana na tuhuma kwamba kiongozi huyu mwenye umri wa miaka 32, amekuwa akitengeneza silaha za nyuklia. Lakini je anaishi wapi na vipi?

Makazi yake?

Taarifa zinazotolewa na vyombo mbali mbali vya habari ndani na nje ya taifa la Korea Kaskazini zinasema kuwa kiongozi huyu anaishi katika nyumba 15 tofauti kwa awamu na makazi anayoishi, wapi yanapopatikana ni siri kubwa inayotunzwa na serikali ya Korea Kaskazini na ni picha chache tu za makazi yake zilizopo.

Kim Jong Un anaaminiwa kuwa na nyumba 15 anazoishi kwa awamu zilizoko kwenye maeneo tofauti ya nchi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kim Jong Un anaaminiwa kuwa na nyumba 15 anazoishi kwa awamu zilizoko kwenye maeneo tofauti ya nchi

Hata hivyo wakati mwaka jana wakati mlipuko wa Covid-19 uliposambaa katika maeneo mengi duniani, inaripotiwa kuwa Kiongozi huyo wa Korea alikwenda kusihi katika makazi yake yaliyoko ufukweni mwa bahari katika eneo la Wonsan.

Makazi yake ya kifahari ya Wonsan yanaripotiwa kuwa ndiyo pekee yenye vidimbwi vya kuogelea, viwanja vya tenisi , maeneo ya kuteleza ndani ya maji na uwanja wa michezo , vyote vikiwa mashariki mwa Korea Kaskazini kwenye fukwe za kuvutia za bahari ya Japan.

Anapenda kula na kunywa nini?

Kim Jong Un ni kiongozi anafahamika kwa kupenda vyakula vya ajabu vya baharini , akipendelea zaidi samaki wa bahari ndogo ya nchi kavu ya gaspi na samaki weusi ambao wanauzwa kwa bei ghali kutoka bahari ya Caspi . Inasemekana samaki wa aina hii ni miongoni mwa viumbe wanaotoweka duniani kutokana na uchache wao.

Kunywa mvinyo na Champagne.

Kim ni mtu anayependa maisha ya raha na pombe anazokunywa ni za bei kali

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kim ni mtu anayependa maisha ya raha na hupenda vinywaji bora vya bei kali

Mbali na vitisho vya kufyatua makombora Kim Jong Un anapenda maisha ya raha na kuvinjari kwa glasi nzuri ya mvinyo. Unaweza kujiuliza ni aina gani ya mvinyo anaukunywa?...Kiongozi wa Korea Kusini Kusini anapendelea mvinyo wa Ufaransa na wakati mmoja aliwahi kujigamba kwamba anaweza kunywa chupa 10 za mvinyo wa bei kali kwa jioni moja. Hata hivyo hakuna aliyethibitisha haya kwani kama ilivyo kwa taarifa mbali mbali zinazotoka Korea Kaskazini mara nyingi ni vigumu kujua nini ni ukweli na nini sio ukweli. Inasemekana pia kwamba anapenda pombe aina ya Vodka kutoka Urusi.

Pombe aina ya Cristal champagne - Champagne inayouzwa kwenye chupa ya glasi, iliyotengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka 1876 na mjasiliamali wa Ufaransa anayeitwa Louis Roederer. Kim Jong Un hupenda champagne, lakini hupendelea aina ya Cristal kwasababu inaaminiwa kuwa ndio bora zaidi. Na inaaminiwa kuwa kinywaji hiki, mvinyo pamoja na vyakula vingine avipendavyo havikosekani katika makazi yake tofauti ya kifahari.

Yuko sawa na baba yake

Baba yake Kim Jong-Un, Kim Jong Il, ambaye alikuwa mtawala wa zamani wa Korea Kaskazini alipenda sana Pizza na alipenda mikate yenye nyama ndani (pies) na burger. Kulingana na mpishi aliyemfanyia kazi katika kituo cha pizza, hiki kilikuwa ni chakula alichokipendelea zaidi Kim. Kim Jong Un pia anafahamika kwa kupenda sana kula Pizza yenye jibini kavu pamoja na nyama zenye mafuta mengi.

Burger

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kim Jong Un (kushoto)akiwa na Rodrigo Duterte , pia hupenda vyakula vya haraka vya kampuni za Mc Donalds na KFC

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kim Jong Un (kushoto)akiwa na Rodrigo Duterte , pia hupenda vyakula vya haraka vya makampuni ya Mc Donalds na KFC, ambavyo inaaminiwa alianza kuvila alipokuwa mwanafunzi mdogo nchini Uswizi

Kim, ambaye ana unene wa mwili wa kupindukia, huagiza kiwango kikubwa cha jibini ya Ufaransa na huvuta sigara za Marekani.

Mbali na mvinyo wa Ufaransa na Vodka ya Urusi, Kim Jong Un hunywa kahawa ya Brazil inayofahamika kama Brazilian joe. Kiongozi huyu wa Korea Kaskazini anayedaiwa kuwa dikteta anaaminiwa kutumia mamia ya dola kila mwaka kununua kahawa hiyo kutoka America Kusini.

Bakuli kubwa la supu

Kim Jong Un anapenda supu ya papa na vile vile nyama yake ambayo ni sehemu ya chakula cha kitamaduni cha Wachina ambapo papa anaweza kuchemshwa na mtu kunywa supu yake au kumla yeye kama nyama na supu yake. Kim anasemekana hunywa supu kwa kutumia bakuli kubwa.

Supu ya Papa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Supu ya Papa

Supu ya papa sio chakula pekee anachokipendelea kiongozi huyu wa Korea Kaskazini, kwani hupenda chakula maarufu cha kichina kiitwacho Suchi . Sushi ni chakula cha muda mrefu kinachopendwa sana barani Asia na mara nyingi huhusishwa na vyakula vyenye kuleta afya, lakini Kim sawa na baba yake hupendelea zaidi eneo lenye mafuta zaidi la samaki aina ya tuna anapokula mlo wa Suchi.

Nyama ya bei kali

Kama unapenda nyama basi utamuelewa Kim Jong Un. Kiongozi huyu wa Korea Kaskazini anasemekana kuwa mraibu wa nyama ya Japan ambayo huwa ni nadra na ghali sana kupatikana ya mifugo kutoka eneo la Wagyu. Nyama hii kwa kawaida huitwa ''nyama ya Kobe'' mji ambapo nyama hii hutoka . Japan ina mfumo wa kipekee wa kuwakuza mifugo ili wawe na nyama ya kiwango cha juu na aina fulani ya ladha na uvimbe wake wenye muundo wa tofali.

Mtindo wa mavazi unaotuma ujumbe

Sawa na watoto wengine wa Korea Kaskazini alivaa vazi lake la Jenerali wa kijeshi kuanzia shuleni akiwa mtoto.

Muonekano wa mavazi huwakilisha ujumbe anaotaka kuufikisha

CHANZO CHA PICHA,EPA

Maelezo ya picha,

Muonekano wa mavazi wa kiongozi wa korea Kaskazini huwakilisha ujumbe anaotaka kuufikisha

Hata hivyo tangu alipochukua hatamu za uongozi ameamua ameamua kuchukua muonekano wa mavazi yanayowasilisha ujumbe wa vile anavyojiona mwenyewe, uongozi wake na nafasi yake katika dunia.

Katika vazi lake la suti anawasilisha ujumbe kuwa anafanana na baba yake Kim Il Sung, kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini, jambo ambalo wachambuzi wengi wanaamini linamfaidi binafsi.

Unaweza pia kusoma:

Huvaa miwani ya mtindo wa mwaka 1950 , na suti za mtindo wa Mao ili kuimarisha muonekan Mao .

Wachambuzi wanasema nguo ya Kim Jong Un inatueleza juu ya kiongozi huyo, nchi yake, na uhusiano wa nchi yake na maadui wake.

Kiongozi wa Korea Kaskazini anafahamika kama kiongozi asiye tafuna maneno

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kiongozi wa Korea Kaskazini anafahamika kama kiongozi asiye tafuna maneno

Hatafuni maneno

Kiongozi wa Korea Kaskazini anafahamika kama kiongozi asiye tafuna maneno anapotaka kutuma ujumbe hususan kwa mataifa ya magharibi na Marekani.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post