Hatma ya mpango wa nyuklia wa Iran haijulikani

0





Makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na mataifa yenye nguvu duniani yako mashakani wakati Iran ikijitayarisha kupiga kura kesho Ijumaa kumchagua rais mpya, huku wanadiplomasia wakiendeleza juhudi zao za kuirejesha Iran na Marekani katika makubaliano hayo. Makubaliano hayo yanawakilisha mafanikio muhimu ya uongozi wa miaka minane wa rais mwenye msimamo wa wastani Hassan Rouhani, ambayo ni pamoja na kusitishwa kwa vikwazo vikali kwa Iran kukubali usimamizi mkali na kupunguza urutubishaji wa madini ya urani. Makubaliano hayo yaliporomoka mwaka 2018 kufuatia uamuzi wa upande mmoja wa rais wa zamani Donald Trump kuiondoa Marekani kwenye mpango huo, na kusababisha mashambulizi na makabiliano katika eneo pana la Mashariki ya Kati. Hatua hii pia iliilaazimu Iran kurutubisha urani kwa viwango vya juu kabisa. Wakati wachambuzi pamoja na uchunguzi wa maoni wakimtabiria ushindi mgombea mwenye msimamo mkali ambaye ni mlengwa wa vikwazo vya Marekani Ebrahim Raisi, huenda kukawa na uwezekano wa kurejea kwa makubaliano hayo, lakini hii yumkini isipelekelee maridhiano zaidi kati ya Iran na mataifa ya Magharibi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable