Korea Kaskazini yajiandaa kwa mazungumzo na makabiliano na Marekani

0


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema nchi yake inatakiwa kujiandaa kwa mazungumzo na makabiliano na Marekani. Kim Jong Un amesema hayo katika mkutano na kamati kuu ya chama tawala cha Wafanyakazi kwamba taifa hilo linatakiwa kujiandaa kikamilifu kwa makabiliano, hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la serikali la KNCA hii leo. Kim amewaambia viongozi waandamizi wa chama hicho kwamba wanatakiwa kulinda heshima ya taifa lao pamoja na maslahi yake kwa ajili ya maendeleo yayiyo huru na ya kuaminika ili kuhakikisha mazingira ya amani na usalama wa taifa. Hata hivyo KNCA hawakueleza ni mwelekeo upi ambao Kim ameuchukua kuelekea Marekani ingawa ilisema aliwasilisha uchambuzi wa kina wa mwonekano wa sera dhidi ya serikali mpya ya Marekani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable