Kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS, limedai kuhusika na mashambulizi ya mabasi madogo mawili yaliowauwa watu 7 katika eneo ambalo wanaishi Washia wengi magharibi mwa Kabul, nchini Afghanistan.Miongoni mwa waliouwawa ni, wafanyakazi wawili wa kampuni ya serikali ya taifa hilo ya kutengeneza filamu. Katika taarifa iliyotolewa jana jioni kundi hilo la IS kwa Afghanistan limesema limeyaripua magari mawili yaliyowabeba waisalmu wa madhehebu ya Shia, wakiwaita "wasio na imani."Kundi hilo limekuwa lifanya mashambulizi yenye kufanana katika eneo hilo, yakiwemo mashambulizi manne ya mabasi madogo manne mapema mwezi huu ambayo yalisababisha vifo vya watu 18.

