Lebanon imeshiriki mgomo wa siku moja kufuatia hali ya kiuchumi kuwa mbaya
Lebanon imeshiriki mgomo wa siku moja, ulioitishwa leo na shirikisho kuu la wafanyakazi, kupinga madhila ya kiuchumi na kisiasa nchini humo. Mgomo huo, unaoungwa mkono na baadhi ya vyama vya kisiasa vilioko madarakani, uliitishwa hasa kupinga hali inayozidi kudorora ya kifedha na ucheleweshwaji wa kuunda serikali. Mitaa kadhaa ya mji mkuu Beirut na barabara kuu muhimu Kusini na Kaskazini mwa nchi hiyo zilifungwa. Mkuu wa Shirikisho kuu la wafanyakazi wa Lebanon, Bachara Al-Asmar, amewatolewa wito wanasiasa wa Lebanon, kuacha malumbano na migawanyiko ili kuunda serikali ya ukombozi wa kitaifa, itakayotatua suala la kiuchumi.

