Homebongo habari Maelfu waandamana Brazil kupinga sera za serikali kuhusu Covid-19 byben -June 20, 2021 0 Maelfu waandamana Brazil kupinga sera za serikali kuhusu Covid-19Maelfu ya watu nchini Brazil walifanya maandamano kote nchini humo jana Jumamosi kulalamika kuhusu jinsi rais wa nchi hiyo Jair Bolsonaro anavyolishughulikia janga la virusi vya corona na kumshtumu kwa kutonunua chanjo za virusi hivyo kwa haraka na pia ukaidi wake dhidi ya kuvaa barakoa.Wizara ya afya nchini humo imesema kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID-19 ilipita watu laki tano hapo jana hiki kikiwa kiwango cha juu zaidi cha vifo duniani baada ya Marekani. Waandamanaji wengi walitaja vifo hivyo kama aina ya mauaji ya halaiki yaliyofanywa na serikali dhidi ya watu wa Brazil. Waliimba na kupiga ngoma huku wakibeba mabango ya kumtaka Bolsonaro kuondolewa madarakani. Serikali ya nchi hiyo inakabiliwa na shtuma kali kwa kutotumia fursa za mapema kununua chanjo. Kampuni ya kutengeneza chanjo ya Pfizer imesema kuwa haikupata jibu kuhusu pendekezo lake la kuiuzia serikali hiyo chanjo kati ya mwezi Agosti na Novemba mwaka jana. Tags bongo habari Facebook Twitter