Mshindano ya Olimpiki Japan: Mwanariadha wa Uganda akutwa na corona

Michezo ya olimpiki

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mwanariadha wa kundi la Olimpiki la Uganda amekuwa mtu wa kwanza kupatikana na virusi vya corona baada ya kuwasili nchini Japan ili kushiriki katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza tarehe 23 mwezi Julai.

Mashindano hayo yaliahirishwa mwaka uliopita , na sasa yanaendelea licha ya wimbi jipya la virusi vya corona nchini Japan.

Uganda inakabiliwa na ongezeko la visa vya maradhi hayo, ambavyo vimelazimu serikali kuimarisha masharti ya kutotoka nje siku ya Ijumaa.

Raia huyo wa Uganda ambaye hakutajwa jina ni miongoni mwa timu ya watu tisa ambao walikuwa wamepewa chanjo , ripoti zinasema.

Kundi hilo ambalo linashirikisha mabondia , makocha na maafisa pia walikuwa hawana corona kabla ya kuondoka Uganda.

Hatahivyo mmoja wao alikutwa na virusi hivyo alipowasili katika uwanja wa ndege wa Narita alinukuliwa wakisema.

Raia hao wa Uganda ni kundi la pili la wanariadha wa kigeni kuwasili kwa mazoezi kabla ya mashindano hayo kuanza .

Kundi la wanariadha wa kike wa Australia liliwasili tarehe mosi mwezi Juni.

Mashabiki wa kigeni wamepigwa marufuku kushiriki katika mashindano hayo.

Uamuzi unatarajiwa kuchukuliwa siku ya Jumatatu kuhusu iwapo kuwaruhusu mashabiki wa nyumbani waingi uwanjani.

Hatahivyo maafisa wengine wa Japan wamesema kwamba wanataka mashabiki wa nyumba kutazama mashindano hayo uwanjani.

Mshindano ya Olimpiki Japan: Mwanariadha wa Uganda akutwa na corona

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mshindano ya Olimpiki Japan: Mwanariadha wa Uganda akutwa na corona

Tokyo iliripoti visa 376 vya corona na kifo kimoja tarehe 20 mwezi Juni , ikiwa ni visa 72 zaidi ya wiki moja iliopita, gazeti la kibinafsi la The Asahi Shumbun liliripoti.

Pingamizi kutoka kwa vyombo vya habari vya nchini kuhusu michezo hiyo inaendelea licha ya uhaba wa chanjo.

Ni asilimia 16 ya idadi ya raia ya Japan ambayo imepokea chanjo kufikia sasa kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

Maafisa na wafanyakazi waliojitolea wanaofanya kazi katika viwanja vya michezo hiyo walianza kupokea chanjo siku ya Ijumaa.

Nchini Uganda, Rais Yoweri Museveni alitangaza marufuku kuhusu usafiri, isipokuwa magari yanayobeba watalii na wafanyakazi wa dharura na wale wanaotoa huduma muhimu.

Pia alifunga shule na vyuo vikuu na maeneo ya kuabudu kwa siku 42.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post