Homebongo habari Mwanamke aliyejawa na furaha baada ya kuzaliwa kwa king'ina katika Edinburgh byben -June 20, 2021 0 CHANZO CHA PICHA,SWNSMaelezo ya picha,(Kutoka Kushoto Kwenda Kulia ) Toni-Leigh, miaka 17, Chyrel, 50, Mary Marshall, 86, Nyla wiki tatu, Rose, 68, na Carrie, 35Mwanamke mmoja mkonge mstaafu wa Uskochi amekuwa bibi wa vinng'ina akiwa na vizazi vyote sita vilivyo hai kwa wakati mmoja.Mary Marshall, 86, ana jumla ya wajukuu 90, vitukuu ,vilembwe , vilembwekeza na king'ina akiwa ni mama wa watoto wanane, kutoka mji wa Edinburgh, ana familia moja pekee yenye hadi vizazi sita.Familia hiyo inaanzia kwa Mary ambaye ndiye mwenye umri mkubwa zaidi hadi kwa Nyla Ferguson, ambaye ana umri wa wiki tatu.Akina mama hao wote wanatoka katika upande moja wa familia -na wote isipokuwa mama wa mtoto mchanga Toni-Leigh Aitken wanafanya kazi , au walifanya kazi, na walezi wa watoto.Wote walijifungua wakiwa na umri wa miaka 18 au chini yake na wanaishi katika eneo la Edinburgh.zawadi za siku ya kuzaliwaMkuu wa familia Mary ana watoto wanane, akiwemo binti yake mkubwa Rose.Rose Thorburn, mwenye umri wa miaka 68, ana watoto wanne, akiwemo mama wa watoto watatu Chyrel Borthwick, mwenye umri wa miaka 50.Chyrel alimzaa mama wa watoto wanne Carrie Dow mwaka 1986.Carrie, mwenye umri wa miaka 35, ana watoto wanne, akiwemo mama mpya Toni-Leigh, mwenye umri wa miaka 17.Tarehe 25 Mei,2021, Mary alipata cheo cha mwanamke pekee aliyepata king'ina Uskochi takiwa hai baada ya kuzaliwa kwa Nyla Ferguson.Kutokana na ukubwa wa familia yake, Mary anasema amesamehewa kwa kutomnunulia kila mmoja wa wanafamilia yake zawadi ya siku ya kuzaliwa na Christmas kwani angetumia "nusu ya mwaka akifanya hivyo ".'Furaha sana'Mary alisema : "Mimi ni mwanamke mwenye bahati, kusema ukweli. Ni furaha kubwa kuwa na familia kubwa kiasi hiki . Kuna mtu unayemuona pale kila mara . Nina furaha kubwa ."Mama mpya, Toni-Leigh, ambaye alijifungua mwanafamilia mpya zaidi mwezi uliopita, anasema: "Tulipogundua kwamba nilikuwa mjamzito, tulifanya mzaha juu ya kuvunja aina fulani ya rekodi."Halafu tukaanza kuangalia suala hilo na ni kama hakuna mtu yeyote katika familia yangu anafanana na mwenzake katika familia yetu." Ni mapema kidogo kuona kama anafanana na bibi yake mkubwa zaidi, lakini walipendana sana walipokutana kwa mara ya kwanza."Tunaishi mwendo wa dakika 15 hadi 20 kwa gari kila mmoja kwahiyo tunaweza kuonana."Aliongeza kuwa kila mara kulikuwa na "kelel kiasi " wakati wanapokutana kama familia waRose, mwenye umri wa miaka 68, alisema: "Ni furaha sana wakati mtoto mchanga anapozaliwa. Mimi ni mmoja kati ya watoto wanane kwahiyo kila mara nimekuwa na familia kubwa."Lakini sasa tuna familia kubwa. Sijawahi kusikia familia yoyote kubwa kiasi hiki Uskochi."Kila mara tunapokusanyika, kunakuwa kila mara na raha na vicheko. Kuna mtu kila wakati pale wa kuzungumza naye ."Familia hiyo inaaminiwa kuwa ndio familia pekee nchini uskochi mwenye vizazi sita vinavyoishi wakati mmoja.Kulingana na rekodi ya dunia ya Guinness , familia yenye vizazi vingi wengi zaidi kuwahi kushuhudiwa hadi leo, ilikuwa na vizazi hadi saba vinavyoishi. Tags bongo habari Facebook Twitter