'Maajabu! Meli yapigwa picha ikiwa 'angani' pwani ya Uingereza

Udanganyifu wa macho ulisababisha meli kuonekana kana kwamba ilikuwa ikitanda juu ya upeo wa macho

CHANZO CHA PICHA,DAVID MORRIS/APEX

Maelezo ya picha,

Udanganyifu wa macho ulisababisha meli kuonekana kana kwamba ilikuwa ikitanda juu ya upeo wa macho

Picha ya kile kinachoonekana kuwa meli ilio angani imenaswa kutokana na hali isio ya kawaida karibu na pwani ya England.

David Morris alipiga picha ya meli hiyo karibu na eneo la Falmouth, Cornwall.

Mwandishi wa masuala ya hewa wa BBC David Braine alisema kwamba uhuishaji huo ulionekana kutokana na hali maalum ya anga ambayo hupinda mwanga.

Anasema kwamba hali hiyo hupatikana sana katika bahari ya Arctic, lakini inaweza kuonekana mara chache nchini Uingereza wakati wa majira ya baridi.

Bwana Moris alisema kwamba alishangazwa aliponasa picha hiyo huku akitazama bahari kutoka alipokuwa.

Bwana Braine alisema: Picha kama hizo hutokea kutokana na hali ya hewa kwa jina 'temperature inversion' ambapo hewa baridi huwa karibu na bahari huku hewa yenye joto ikiwa juu yake.

Kwasababu hewa baridi ni nzito kuliko hewa yenye joto, hupinda mwangaza unaokaribia macho ya mtu aliye ardhini ama katika pwani na kubadilisha muonekano wa kitu.

Meli inayoelea angani yapigwa picha Cornwell

CHANZO CHA PICHA,DAVID MORRIS/APEX

Maelezo ya picha,

David Morris alipiga picha hiyo karibu na eneo la Falmouth

"Picha kama hizo zinaweza kuwa aina tofauti - hapa meli hii inaonekana ikiolea juu ya eneo lake , lakini wakati mwingine kitu kilicho chini ya upeo wa macho kinaweza kuonekana.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post