Steven Pladl alihamia mji mmoja huko North Carolina, nchini Marekani, mwaka jana kuanza maisha ya kimapenzi na binti yake Katie Rose Fusco.
Baada ya kuishi pamoja kwa miezi kadha kama wachumba, walijaribu kuhalalisha ndoa yao, lakini kufikia mwisho wa mwezi Januari mwaka jana walikamatwa.
Sasa wanakabiliwa na mashtaka ya kuwa na uchumba wa jamaa wa familia moja, uzinzi na kupanga kufanya uhalifu, kwasababu Pladl, 42, ni baba mzazi wa Fusco, 20.
Mwaka 1998, mara baada ya kuzaliwa mtoto huyo mdogo wa kike aliasiliwa. Alipofikisha umri wa miaka 18, mwaka 2016, aliwatafuta wazazi wake asili na kuamua kwenda kuishi nao mjini Richmond, Virginia, mashariki mwa Marekani.
Mke wa Pladl aliondoka nyumbani alipogundua anashiriki ngono na binti yao. Baadaye alipiga ripoti alipogundua kuwa Fusco ni mjamzito.
Sheria za North Carolina na Virginia zinaharamisha uhusiano kama huo na adhabu yake ni kifungo gerezani. Wale wanaovunja sheria hiyo ,wakipatikana na hatia wanakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 gerezani.
Kando na New Jersey na Rhode Island, nchini Marekani uchumba kati ya watu wa familia moja ni hatia. Hata hivyo kuna nchi kadhaa ambazo zinaruhusu mahusiano kama hayo.
Ni wapi uhusiano wa ndugu wa damu unaruhusiwa?
Nchi kadhaa zilizoendelea hazina sheria zinazodhibiti uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wawili wazima walio na uhusiano wa kifamilia wa moja kwa moja au wa mbali, hali inayochangia uhusiano wa kimapenzi kati ya wanafamilia.
Hata hivyo katika nchi hizo kuna sheria zinazozuia uhusiano wa kimapenzi kati ya mtu mzima na mtoto ambaye ni wa familia yake, na huchukuliwa kama ubakaji.
Nchini Uhispania kwa mfano, uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa familia moja unaruhusiwa, ijapokuwa ndoa kati ya watu wazima walio na uhusiano wa kifamilia hairuhusiwi: mjomba hawezi kumuoa mpwa wake.
Kwa upande mwingine, nchini Ureno ndoa kati ya mandugu imeharamishwa lakini mjomba anaweza kuoana na mpwa wake.
Nchini Ufaransa sheria inasema kwamba ndoa inaweza kuidhinishwa na agizo la rais kati ya wakwe. Wakati mtu aliyeanzisha uhusiano huo amekufa.
China, Japan na Urusi ni nchi zingine ambazo hazijaharamisha ndoa kati ya watu wa familia moja lakini ndoa ya kisheria inadhibiti uhusiano kama huo..
Nchini Sweden ndoa kati ya ndugu wa kambo ambao wana baba wa pamoja inaruhusiwa. Lakini kwa hili wanahitaji idhini maalum kutoka kwa serikali.
Nchini Uholanzi uhusiano wa aina hiyo haujakatazwa lakini ndoa kati ya ndugu waliozaliwa pamoja imezuiliwa, na ndoa inayohusisha jamaa wa mbali wa familia moja sharti izingatie muogozo wa sheria.
Katika nchi zingine uchumba kati ya watu wa familia moja umeidhinishwa alimradi wahusika ni watu wazima waliokubaliana kwa hiari.
Brazili ni moja nchi zinazokurusu uhusiano wa aina hiyo iwapo wahusika wamekubaliana, lakini katika nchi hiyo ya Amerika Kusini sheria imeharamisha uhusiano wa kimapenzi kati ya mtu mzima na watoto hata kama ni wa familia moja.
Nchini Italia na Uruguay, sheria zao zinatoa adhabu kwa uhusiano wa aina hiyo kama"kashfa ya umma" , maana ya halisi ya maneno hayo yanachanganya kwani haielezei "kashfa" ni nini hasa.
Australia ni nchi iliyo na sheria kali dhidi ya uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa familia moja, ambapo mtuhumiwa anaweza kuzuiliwa jela kwa zaidi ya miaka 20 akipatikana na hatia.
Vitendo ya mahusiano baina ya ndugu wa damu vilianza siku nyingi, toka katika kale za ustaarabu wa watu wa kale kuanzia Misri, Ugiriki mpaka Roma. Hata hivyo vikaanza kupigwa marufuku baada ya warumi kutengeneza sheria.
Carlos Welti, Profesa wa Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Chicago, anaelezea kuwa kuzuia uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa familia moja ni wajibu wa kisheria kulinda familia na msingi wake katika jamii.
"Kuzuia uchumba wa aina hii kunachangia usatawi wa familia, kwani inabainisha wazi majukumu ambayo kila mmoja anapaswa kutekeleza," Welti alielezea BBC.
"Katika mahusiano ya jamaa ni vigumu sana kubainisha majukumu ya kila mmoja wao. Mpenzi wa ndoa ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na binti, au mama na mtoto wa kiume, hugubika majukumu hayo," anaongeza.
Pamoja na hayo, mtaalam huyo anakubali kuwa kuna nchi ambazo zinaharamisha uhusiano wa aina hiyo kwa lengo la kuwalinda wahanga wa unyanyasaji wa kijinsia.
Kutoweadhibu husaidia watu ambao wana uhusiano ambao hawakubaliani na kuripoti kwa urahisi, hawaogopi kushtakiwa kwa uchumba au kufungwa gerezani.
Wanaopinga sheria zinazodhibiti uhusianao wa kimapenzi kati ya ndugu wa damu wanachukulia uhusiano huo kama uhuru wa kijinsia kati kati ya watu waziama.
Kwao sheria zinazopinga mahusiano hayo zinategemea dhana za maadili.
Athari za mahusiano ya ndugu wa damu ni zipi?
Kando na hatua za kisheria kudhibiti mahusiano ya ndugu wa damu, mahusiano hayo yanakabiliwa na changamoto hasa mtoto anapozaliwa.
Utafiti unaonesha kuwa Czechoslovakia ya zamani ni kisa cha nadharia cha uchumba wa damu.
Miongoni mwa watoto waliozaliwa kati ya mwaka 1933 na 1970 kutokana na wazazi ambao ni ndugu wa damu- Asilimia 40 walikuwa na ulemavu na mmoja katika asilimia 14 alifariki.
Dr. Debra Lieberman, mtaalamu wa masuala hayo katika Chuo Kikuu cha Miami, anaelezea kwamba kuzaa na ndugu wa damu au jamaa " kunaongeza uwezekano wa kupata jeni mbili zenye hitilafu ikilinganishwa na kuzaa na mtu kutoka nje ya familia."
Kwa hivyo, uhusiano wa ndugu wa damu, hata kama washiriki wanakubaliana nao, mara nyingi huanza kutoka kwa nafasi ushawishi na nguvu ya familia.
"Kwa kweli, uhusiano wa jamaa ni dhihirisho la unyanyasaji kati ya watu ambapo uhusiano wa nguvu ni sawa," anasema mtaalam wa kijamii Carlos Welti.
Pia anaongeza kuwa kuna tafiti ambazo zinaonyesha kwamba kuna "utaratibu" wa kibaolojia ambao husababisha wanadamu kuwa na "chuki za kijinsia" kwa wazazi na ndugu.