Homebongo habari Profesa Mkenda awataka wafanyabiashara kuwekeza kwenye mbolea byben -June 14, 2021 0 Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Profesa Adolf Mkenda amewataka wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kufanya biashara ya mbolea. Amesema mahitaji ya mbolea nchini ni takribani tani 700,000 lakini uzalishaji wake ni chini ya tani 100,000.Profesa Mkenda ameyasema hayo leo Jumatatu Juni 14, 2021 alipofanya ziara Bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kuangalia shughuli ya upakuaji wa mbolea na kuingiza ndani ya nchi."Nichukue fursa hii kuwaita wafanyabiashara wa Tanzania na wa nje ya nchi. Ningependa hasa nchi zile zenye mbolea waongeze ushindani ili mbolea ishuke na niwaambie Watanzania kwenye mbolea kuna biashara njooni tengenezeni fedha kwa kuagiza mbolea.”"Kama tukichunguza unaweza kuingiza mbolea basi wewe ndio utapewa tenda ya kuingiza mbolea na hatutanunua mbolea ya mtu mwingine mpaka tuhakikishe ya kwako imeisha," amesema. Tags bongo habari Facebook Twitter
Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Profesa Adolf Mkenda amewataka wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kufanya biashara ya mbolea. Amesema mahitaji ya mbolea nchini ni takribani tani 700,000 lakini uzalishaji wake ni chini ya tani 100,000.Profesa Mkenda ameyasema hayo leo Jumatatu Juni 14, 2021 alipofanya ziara Bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kuangalia shughuli ya upakuaji wa mbolea na kuingiza ndani ya nchi."Nichukue fursa hii kuwaita wafanyabiashara wa Tanzania na wa nje ya nchi. Ningependa hasa nchi zile zenye mbolea waongeze ushindani ili mbolea ishuke na niwaambie Watanzania kwenye mbolea kuna biashara njooni tengenezeni fedha kwa kuagiza mbolea.”"Kama tukichunguza unaweza kuingiza mbolea basi wewe ndio utapewa tenda ya kuingiza mbolea na hatutanunua mbolea ya mtu mwingine mpaka tuhakikishe ya kwako imeisha," amesema.