Wanachama AAAM watembelea kiwanda cha magari Tanzania



Dar es Salaam. Wanachama wa umoja wa watengenezaji wa magari duniani (AAAM) wametembelea kiwanda cha magari cha GFA Kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Wakiwa nchini Tanzania wamekutana na viongozi wa Serikali na kuzungumza mambo kadhaa kuhakikisha lengo la Tanzania ya viwanda linatimia kwa vitendo.

Kiongozi wa msafara huo ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Nissan ukanda wa Afrika ,Mike Whitfield  amesema watashirikiana na kiwanda hicho cha GFA katika maeneo mbalimbali ili kiweze kujitegemea katika uunganishaji wa magari ili Tanzania kuwa kama nchi nyingine zinazotengeneza magari kama  Afrika Kusini.

magarinyinginepicc

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa   kampuni ya GFA, Mehbooub Karmali ameshukuru ujio wa wanachama hao akibainisha kuwa wakiweza kufanya kila kitu katika kiwanda hicho itakuwa faida kwa Taifa.

Miongoni mwa wanachama wa umoja huo ni Nissan, Ford, BMW, Isuzu, Toyota na Volkswagen.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post