Homebongo habari Iluminati: Mambo kumi kuhusu jamii ya kisiri kuwahi kuonekana duniani byben -June 14, 2021 0 Maelezo ya picha,Nembo ya Iluminati wa piliokuwa Bavaria ambayo sasa ni UjerumaniIlluminati ni jina lililopatiwa jamii iliobuniwa miaka 245 iliopita.Jamii hiyo ilizua nadharia kwa miaka mingi , huku watu wakidai kwamba ni shirika moja la kisiri ambalo nia yake ni kuteka uuongozi wa dunia.Mbali na kuwa chanzo cha mapinduzi makubwa duniani na mauaji. Lakini Illimunati ni akina nani na je ni kweli walidhibiti ulimwengu?Hi ki ndicho tunachokijua kuhusu mojawapo ya jamii za siri zinazovutia zaid katika historia.1. Je ni akina nani walioanzisha IlluminatiJamii ya iluminati ilikuwa jamii ya siri iliobuniwa nchini Bavaria kwa sasa Ujerumani ambapo ilikuwepo kuanzia 1776 hadi 1785 ambapo wanachama wake walikuwa wakijiita wakamilifu.Kundi hilo lilianzishwa na Profesa wa sheria Adam Weishaupt. Alitaka kukuza elimu ya fikra ili kupinga uchawi na ushawishi wa kidni katika jamii.Weishaupt alitaka kubadilisha jinsi serikali zilivyoendeshwa barani ulaya , akiondoa ushawishi wa kidini katika serikali na kuwapatia walimwengu muongozo mpya .Inaaminika kwamba mkutano wa kwanza wa iluminati huko Bavarian ulifanyika katika msitu karibu na Ingolstadt mwezi Mei tarehe mosi 1776.Wakati huo, watu watano walianzisha sheria ambazo zingetawala siri ya utawala wa Iluminati.Kwa muda sasa, lengo la kundi hilo liliangazia kuhusu kushawishi maamuzi ya kisiasa na kumaliza taasisi kama zile za kifalme na kanisa.Baadhi ya wanachama wa Iluminati walijiunga na kundi la Freemasons ili kusajili wanachama wapya.Ndege mmoja anayejulikana kama Minerva Owl alitumika kuwa nembo yake.CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESMaelezo ya picha,Ndege huyo alikuwa mnyama mtakatifu wa mungu wa kike Athens katika hadithi za Uigiriki, na katika tamaduni za Kirumi, ndege wa Minerva.2.Je iluminati wanahusiana vipi na Freemasons?Masoni ni agizo la kindugu ambalo lilikua kutoka kwa vikundi vya waashi wa mawe na wajenzi wa kanisa kuu la zama za Kati.Katika nchi zingine, haswa Marekani, kihistoria kumekuwa na hisia fulani kuhusu Freemason; Mnamo 1828, harakati moja ya kisiasa inayojulikana kama Chama cha Kupambana na Mason ilianzishwa .Kwa sababu awali Illuminati iliwasajili Freemason, vikundi hivyo viwili mara nyingi vilishukiwa kuwa na uhusiano.3.Je unawezaje kujiunga na Iluminati?Kujiunga na Illuminati, ilibidi uwe na idhini kamili ya washiriki wengine, umiliki mali, na uwe na sifa nzuri ndani ya familia yenye sifa.Kwa kuongezea, kulikuwa na mfumo wa ngazi ya juu kwa ushirika wa Illuminati.Baada ya kuingia kama 'chipukizi', ungehitimu kama "minerval" na kisha "kupanda ngazi ya minerval mkuu", Ingawa muundo huu ulikuwa mgumu zaidi, mtu alihitaji takriban digrii 13 za kuwa mwanachama.CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESMaelezo ya picha,Katika karne ya 19 kulikuwa na picha za Iluminati wakifanya matambiko , hatahivyo ni habari chache zilizosalia kuhusu ukweli wa sherehe hiyo4.Je iluminati ilitumia matambiko haya?Walitumia matambiko - ingawa mengi hayajulikani - na walitumia majina bandia kuweka vitambulisho vya wanachama siri.Walakini, kwa sababu ya nyaraka za siri zilizopatikana, inajulikana jinsi chipukizi wa kundi hilo walivyoweza kupanda hadi nyadhfa za juu ndani ya uongozi wa Illuminati:ilibidi wakusanye ripoti kuhusu vitabu vyote walivyomiliki, na kuandika orodha ya udhaifu wao,na kufunua majina ya maadui waliokuwa nao.Chipukizi hao baadaye waliahidi kuweka maslahi yao na yale ya kibinafsi nyuma na kujitolea kuhudumia jamii hiyo.5.Je jicho linalotumiwa na iluminati lina maana gani?"Jicho la majaliwa," ni ishara inayofanana na jicho ndani ya pembetatu, ambalo linaonekana kwenye makanisa kote ulimwenguni, na vile vile kwenye majengo ya Masoni na kwenye noti ya sarafu ya dola ya Marekani .Mbali na kuhusishwa na Freemasonry, pia imehusishwa na Illuminati kama ishara ya udhibiti wa kikundi na kufuatilia ulimwengu.CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESMaelezo ya picha,Piramidi na jicho linaloona kila kitu , ni nembo iliotumika katika chapa kuu ya MarekaniNi nembo ya Kikristo, "jicho ambalo linaona kila kitu" limetumika katika picha za kuchorwa kuwakilisha umakini wa Mungu juu ya ubinadamu.Hakuna uhusiano rasmi kati ya jicho linaloona yote na Illuminati; uhusiano uliopo pengine ni kwa sababu ya ukweli kwamba kikundi cha asili kilishirikiana na Masoni, ambao walitumia picha hiyo kama ishara ya Mungu.6. Je Illuminati imeitawala dunia?Baadhi ya watu wanaamini kuwa Illuminati inaiongoza dunia hii leo, ambapo ni sawa na kusema kuwa wanachama wao ni wameficha siri yao kwa nguvu zote kiasi cha kwamba ni watu wachache sana wanaijua.Jinsi wanachama wengi wa Illuminati walivyojiingiza kisiri ndani ya Freemason na wale wa Freemason kujiingiza katika Illuminati, ni kazi ngumu sana kupima mafanikio ya Illuminati, lakini wanahistoria wengi wanaamini kundi la asili kabisa la Iluminati liliweza kuwa na ushawishi wa kadri.7. Je kumewahi kutokea wanachama maarufu wa Illuminati?Kufikia mwaka 1782, Illuminati ilifikia kuwa na wanachama 600, ikiwemo mabwanyenye wa Kijerumani kama Baron Adolph von Knigge, ambaye akiwa mwanachama wa zamani wa Freemason, alisaidia Illuminati mikakati na kutapakaa kwa jumuiya hiyo.Awali, wanafunzi wa Weishaupt walikuwa ndiyo wanachama pekee wa Illuminati, lakini baadaye madaktari, wanasheria na wanazuoni wakajiunga.Kufikia mwaka 1784 kulikuwa na wanachama baina ya 2,000 na 3,000 wa Illuminati. Baadhi ya vyanzo vinadai kuwa mwandishi maarufu Johann Wolfgang von Goethe pia alijiunga na Illuminati, japo suala hilo bado lina utata.8. Kwa nini Illuminati ilitoweka?Mwaka 1784, Karl Theodor, Mtawala wa Bavaria, alipiga marufuku uanzishwaji wa chama chochote ambacho hakikutambuliwa kisheria na mwaka uliofuata akapitisha amri mahususi wa kuzuia Illuminati.Wakati wa kamatakamata ya washukiwa wa uanachama wa Illuminati, walikutwa na nyaraka kadhaa ambazo zilikuwa zikipiga chapuo masuala yaliyokuwa yakipigwa vita kama vile kutokuamini katika uwepo wa Mungu, kujiua na namna ya kutoa mimba.Nyaraka hizo zikapigilia msumari imani ya kwamba Illuminati ilikuwa ni jumuiya ya tishio dhidi ya serikali na kanisa.Baada ya hapo, jumuiya ya Illuminati inaaminika kuwa ilipotea, japo baadhi ya watu wanaamini jumuiya hiyo iliendelea kudumu.9. Adam Weishaupt aliishia wapi?CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESMaelezo ya picha,Je mwanzilishi wa kundi hilo Adam Weishaupt aliishia wapi?Adam Weishaupt hatimaye aliondoshwa katika Chuo Kikuu cha Ingolstadt.Baada ya kutimuliwa Bavaria, aliishi siku zake za mwisho huko Gotha, Thuringia, na kufariki dunia mwaka 1830.10. Kwa nini hadithi ya Illuminati imeendelea kuwa maarufu?Toka kipindi ambacho kundi hilo lilipigwa marufuku, Imani za uwongo kuwahusu zimepata umaarifu sana na kusambaa kama moto wa nyika.Mwaka 1797, padre maarufu kutoka Ufaransa Jesuit Abbé Augustin Barruel alidai kuwa jumuiya za siri kama Illuminati zilichochea mapinduzi ya Ufaransa.Rais wa kwanza wa Marekani, George Washington, aliandika barua mwaka mmoja baadaye akisema naamini tishio la Illuminati lilikuwa limedhibitiwa. Barua hiyo ilichangia Imani ya kuwa kundi hilo bado lilikuwa hai.Baadaye vitabu na hotuba za kulishutumu kundi hilo vilitapakaa, huku rais wa tatu wa Marekani Thomas Jefferson, akituhumiw kimakosa kuwa mwanachama wa kundi hilo. Tags bongo habari Facebook Twitter