Homebongo habariTetesi za soka Ulaya Jumatano 16.06.2021: Sterling, Silva, Ronaldo, Dembele, Ramsey, Onana, Welbeck, Ramos Tetesi za soka Ulaya Jumatano 16.06.2021: Sterling, Silva, Ronaldo, Dembele, Ramsey, Onana, Welbeck, Ramos 0 ben June 16, 2021 CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESWinga wa England Raheem Sterling, 26, anatarajiwa kusalia Manchester City msimu ujao, licha ya kuhusishwa kwake kutaka kuondoka kwa mabingwa hao wa ligi kuu England. (Manchester Evening News)Kiungo wa Manchester City Bernardo Silva, 26, angependelea kutimka msimu huu lakini Meneja Pep Guardiola amegoma kumruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno kuondoka. (Athletic - subscription required)Manchester United imepeleka dau la mwaka mmoja la £17m kwa ajili ya kumrejesha mshambuliaji wa kireno, Cristiano Ronaldo kutoka Juventus, katika mpango ambao utashuhudia kiungo Mfaransa, Paul Pogba, 28, akienda upande wa pili. Hata hivyo, chaguo la Ronaldo ni klabu ya Paris St-Germain. (Gazzetta dello Sport, via Mail)CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESJuventus inatarajiwa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa kiungo Aaron Ramsey, 30, kujaribu kutafuta namna ya kuachana na nyota huyo wa kimataifa wa Wales, ingawa mpaka sasa hakuna mawasiliano na klabu yake ya zamani ya Arsenal. (Goal)Barcelona imefanya mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Ufaransa, Ousmane Dembele, kuhusu kuongeza mkataba nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, lakini hakuna hatua yoyote iliyopigwa katika kikao cha kwanza. (Marca)Arsenal wanamuangalia mlinda mlango wa Ajax Andre Onana, 25, lakini bado hawajepeleka 'ofa' yoyote kwa Mcameroon huyo ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi tisa. (Goal)Anderlecht imekataa dau la £13.5m kutoka Arsenal kwa ajili ya kiungo kinda wa kibelgiji Albert Sambi Lokonga, 21, ambapo inataka dau linalokaribia £18m. (Mail)CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESBrighton inataka kumuongezea mkataba, mshambuliaji Danny Welbeck,wako kwenye mazungumzo na muingereza huyo mwenye miaka 30. (Brighton Argus)Winga wa Ufaransa Kingsley Coman, ambaye anahusishwa kutaka kuhamia Manchester United, hatarajiwi kuondoka Bayern Munich kwani yuko kwenye mipango ya meneja Julian Nagelsmann na ili kumuachia klabu hiyo inataka dau nono la £60m kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25. (Goal)CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGESMkurugenzi wa michezo wa Sevilla Monchi amepuuzilia mbali tetesi kwamba mlinzi wa kati wa Hispania Sergio Ramos atarejea klabuni hapo na kusema anafikiri mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35 yuko kwenye mazungumzo na klabu yake ya Real Madrid ili kusalia Klabuni hapo". (Sky Italia, via Marca)Meneja wa Fulham Scott Parker anatarajiwa kuikacha klabu hiyo wiki hii huku Bournemouth ikimtaka kwa udi na uvumba ili awe meneja mpya wa klabu hiyo ya Championship. (Telegraph)Fulham yenyewe imewaorodhesha warithi wa Parker akiwemo meneja wa Swansea City Steve Cooper, Meneja wa Barnsley Valerien Ismael na kocha msaidizi wa zamani wa Fulham Javier Pereira. (90 Min)Klabu za Norwich City na Southampton ni miongoni mwa vilabu vinavyomsaka kwa udi na uvumba mshambuliaji wa Blackburn Rovers Adam Armstrong, 24, ambaye amebakiza mwaka mmoja wa mkataba wake pale Ewood Park. (Mail) Tags bongo habari Newer Older