Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 28.06.2021: Griezmann, Kane, Lingard, Coman, Bellerin, Hakimi

 

Antoine Griezman

CHANZO CHA PICHA,EPA

Manchester City huenda wakamlenga mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Antoine Griezman , 30 kama mbadala wa mshambuliaji wa England na Tottenham Harry Kane.(Fichajes, in Spanish)

Manchester United imempatia Jesse Lingard kandarasi mpya ya miaka mitatu huku kiungo huyo wa England akiwavutia West Ham. (Mirror)

Liverpool ina hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Bayern Munich na Ufaransa Kingsley Coman na inawasiliana na usimamizi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Sport 1 via Metro)

Inter Milan wamewasiliana na wakala wa beki wa kulia wa Arsenal Hector Baellerin huku klabu hiyo ya Itali ikimlenga mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Uhispania atakayechukua mahala pake Achraf Hakimi. (Gianluca di Marzio, in Itali.

Hakimi Achraf

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kiungo wa kati wa Arsenal na Switzerland Granit Xhaka amethibitisha kuondoka katika klabu hiyo ya ligi ya premia kuelekea AS Roma wakati wa mkutano wa kombe la Euro 2020.. (90 min)

Manchester United wanakutana na wakala wa kiungo wa kati wa Rennes 18, Eduardo Camavinga wiki ijayo kuandikisha kandarasi. (RMC, via Mirror)

Kiungo wa kati wa West Ham Felipe Anderson huenda akarudi Lazio baada ya klabu hiyo kuanzisha mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 28.. (Mail)

Felippe Anderson

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Klabu ya Borussia Dortmund itamlenga mshambuliaji wa PSV Eindhoven na England Noni Madueke, 19, kuchukua nafasi itakayowachwa wazi na Jadon Sancho ambaye anatarajiwa kutia saini kandarasi ya dau la £77m na klabu ya Manchester United . (Ruhr Nachrichten, in German)

Southampton inakaribia kukamilisha kumsaini beki wa klabu ya Brests na Ufaransa Romain Perraud, 23, na pia wana hamu ya mshambuliaji wa Blackburn Rovers Adam Armstrong ,24. (Athletic, subscription required)

Miaka miwili baada ya kukataa kujiunga na Arsenal, kiungo wa kati wa Leicester na Ubelgiji Dennis Praett 27, huenda akasajiliwa na klabu hiyo katika dirisha hili la uhamisho. (Express)

Dennis Praet

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Beki wa Brighton na England Ben White, 23, anasema kwamba hajui kile ambacho ni kweli kuhusu uvumi kwamba anaelekea kujiunga na Arsenal kwa dau la £50m. (TalkSport)

Arsenal wameonesha hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa lille na Portugal Renato Sanchez na wameitaka klabu hiyo ya Ufaransa kuipatia habari zozote kumuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.. (90 min)

Liverpool imekataa ombi la klabu ya Uswizi ya FC Basel kumnunua mshambuliaji wa Canada mwenye umri wa miaka 21- Liam Millar na inataka kulipwa fedha za ziada za £1m ili kumuuza mshambuliaji huyo.* (Goal)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post