Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 24.07.2021: Grealish, Haaland, Lukaku, Kane, Pogba, Mbappe, Camavinga

 

Jack Grealish

CHANZO CHA PICHA,PA MEDIA

Manchester City wameafikia makubaliano na kiungo Jack Grealish na iko tayari kuipatia ofa ya £90m Aston Villa ili kumsajli mchezaji huyo wa England, 25. (Football Insider)

Chelsea inatarajiwa kutoa dau la £130m kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 22, baada ya mmiliki wake Roman Abrahamovich kutoa baraka zake kuendelea na kile ambacho kitakuwa rekodi mpya ya klabu hiyo.. (Football Insider)

Inter Milan inataka dau lisilo chini ya £102.5m kutoka Chelsea ili kumuuza mshambuliaji wa Ubeligiji Romelu Lukaku, 28, iwapo The Blues watashindwa kumsajili Haaland. (Metro)

Halaand Braut

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Manchester City inasema kwamba ripoti zinazosema kwamba klabu hiyo imeafikiana na Tottenham kumsaini mshambuliaji wa England Harry Kane kwa dau la £160m ni upuzi (Manchester Evening News)

harry kane

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Tottenham imesisitiza kwamba haina mpango wa kumuuza nahodha huyo wa timu ya taifa ya England msimu huu. (Football London)

Hatahivyo Kane ana matumaini kwamba Tottenham iko tayari kumwachilia kuondoka. (Times)

Manchester City imefanya makubaliano ya kibinafsi na Harry Kane ambaye atakuwa analipwa £350,000 kwa wiki na iko tayari kulipa zaidi ya £120m. (Star)

Manchester United inasubiri ombi kutoka kwa PSG msimu huu la kumtaka kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 28. (Telegraph)

Maelezo ya video,

Jinsi kimbunga kikali cha vumbi kilivyositisha mechi ya kandanda Bolivia

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, ameiambia PSG kwamba hatoongeza kandarasi yake ambayo inakamilika 2022, na hivyobasi anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu huu.. (AS - in Spanish)

Kylian Mbappe

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kiungo wa kati wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga anataka kuhamia Uhispania baada ya mazungumzo kati ya Manchester United na wawakilishi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 kutofua dafu. ". (Manchester Evening News)

Barcelona inaamini kwamba iwapo mshambuliaji wa Portugal Cristiano Ronaldo ataondoka Juventus msimu huu, klabu hiyo ya Itali itakuwa tayari kumnunua kwa mkopo mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann kukiwa na sheria ya kumnunua kabisa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Sport - in Spanish)

Rais wa Barca Joan Laporta anasema kwamba klabu hiyo inamthamini sana Antoine lakini kuna soko lake na kwamba mabingwa hao wa Uhispania wako tayari kwa mapendekezo yote. (Goal)

Arsenal haitamuongezea kandarasi mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette na imetoa ofa ya dau la £15m kwa mchezaji huyo ili kusaidia timu hiyo kupata fedha za kumnunua mshambuliaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23 Tammy Abraham.. (Sun)

Alexander Lacazzette

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mkufunzi wa Newcastle United Steve Bruce amesisitiza kuhusu mpango wa klabu hiyo kumsaini kiungo wa kati wa Arsenal mwenye umri wa miaka 21 Joe Willock lakini inasema kwamba klabu hiyo inasubiri Arsenal na Willock kufanya uamuzi kuhusu hatma yake. (Sky Sports)

Mkufunzi wa klabu ya Rangers na aliyekuwa nahodha ya klabu ya Liverpool Steven Gerrard, 41, amesema kwamba alishangazwa baada ya kuhusishwa na kazi ya kuifunza Everton kabla ya usajili wa Rafael Benitez na kwamba mpango kama huo hauwezekani. ". (ESPN)

Liverpool inataka kumzuia mshambuliaji Mohamed Salah, 29, kuweka kandarasi mpya huku kandarasi ya raia huyo wa Misri ikitarajiwa kukamilika 2023. (Liverpool Echo)

Fulham inakaribia kumsajili winga wa Liverpool na Wales Harry Wilson kwa dau la £10m. (Sun)

Bayer Leverkusen imekataa dau la pauni 30m kutoka kwa Aston Villa kumnunua winga wa Jamaica mweye umri wa miaka 23 Leon Bailey. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Manchester City na Brazil mwenye umri wa miaka 24 Gabriel Jesus ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Juventus msimu huu. (Calciomercator - in Italian)

Gabriel Jesus

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Juve pia inapanga kuzindua jaribio la kumsajili kiungo wa kati wa Sassuolo Manuel Locatelli 23.. (Mail)

Wakala wa mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala anatarajiwa kufanya mazungumzo na klabu hiyo kuhusu kandarasi mpya ya mchezaji huyo ambaye amesalia na mwaka mmoja katika klabu hiyo. (Calciomercato - in Italian)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post