Jadon Sancho akamilisha uhamisho wa kujiunga na Man United kwa dau la £73m

 

Jadon Sancho

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Winga wa England Jadon Sancho anasema kwamba kujiunga na Man United ni ndoto iliotimia baada ya kukamilisha uhamisho kutoka klabu ya Borussia Dortmund kwa dau la £73m.

Sancho ndiye mchezaji wa pili wa England mwenye thamani ya juu baada ya mchezaji mwenza wa United Harry Maguire.

Anajiunga na United kwa kandarasi ya miaka mitano.

  • "Naishukuru Dortmund kwa kunipatia fursa ya kucheza katika kikosi cha kwanza , ijapokuwa , nilijua kwamba nitarudi England'' , alisema Sancho mwenye umri wa miaka 21.

Fursa ya kujiunga na Manchester United ni ndoto iliotimia na sasa nasubiri kuonesha umahiri wangu katika ligi ya Premia''.

"Hiki ni kikosi kichanga na najua , pamoja tunaweza kujenga kitu maalum ili kuleta ufanisi ambao mashabiki wanahitaji.."

United waliafikia makubaliano ya kumsajili Sancho tarehe mosi mwezi Julai na kandarasi yake ya miaka mitano na klabu hiyo ina kifungu cha miezi mingine 12.

Mkufunzi wa Man United Ole Gunar Solskjaer

CHANZO CHA PICHA,JADON SANCHO/TWITTER

Maelezo ya picha,

Mkufunzi wa Man United Ole Gunar Solskjaer

Ukamilishaji wa makubaliano hayo unasitisha uwindaji wa kumsajili mchezaji huyo. Walitarajiwa kumsajili msimu uliokwisha lakini wakatofautiana kuhusu dau la uhamisho wake.

Sancho alifunga magoli 50 na kutoa usaidizi wa magoli 57 katika mechi 137 alizochezea Dortmund.

Mkufunzi wa United Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba Old Trafford itampatia Sancho , fursa anayohitaji kuonesha talanta yake.

"Jadon ni aina ya mchezaji ambaye nilipenda kumleta katika klabu hii - ni mshambuliaji anayeingiliana na utamaduni wa Man United'' , Solskjaer aliambia tovuti ya klabu hiyo.

"Atakuwa kiungo muhimu wa kikosi changu kwa miaka kadhaa ijayo na tunataraji kwamba atang'ara. Magoli yake na rekodi yake ya usaidizi wa magoli ni ya kipekee na pia atatuongezea kasi katika mchezo wetu , umahiri na ubunifu katika timu."

Kurudi kwa Sancho katika ligi ya Uingereza kunajiri baada ya kuisadia timu ya taifa kufuzu katika fainali ya kombe la Yuro 2020 , ambapo walishindwa na Itali kwa penalti.

Mchezaji huyo wa zamani wa Kikosi cha vijana cha timu ya Man City pamoja na Bukayo Saka na Marcus Rashford walikabiliwa na ubaguzi wa rangi katika mitandao ya kijamii baada ya kushindwa kufunga penalti muhimu walizopewa.

Je Sancho analinganishwaje na washambuliaji wa Man United?

Kutoka kushoto ni Rashford, Martial, Greenwood na kulia Cavani

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kutoka kushoto ni Rashford, Martial, Greenwood na kulia Cavani

Sancho anatarajiwa kujiunga na kitengo cha mashambulizi cha United ambacho tayari kinaogopwa msimu ujao.

Image..attackers

Uhamisho wa Sancho katika klabu ya United utamfanya kushirikiana na Rashford, lakini pia Edinson Cavani, Anthony Martial na Mason Greenwood katika kile ambacho kinatarajiwa kuwa kitengo bora cha ushambuliaji.

Sancho alifunga magoli 16 katika mashindano yote wakati wa msimu wa 2020-21 , ikiwa ni magoli matano chini ya Rashford, lakini manne zaidi ya Greenwood na tisa zaidi ya Martial.

Cavani ambaye alijiunga na United kwa uhamisho wa bila malipo mwaka uliopita baada ya kuondoka PSG alifunga magoli 17.

Katika misumu yake minne akiichezea Dortmund , Sancho alitoa usaidizi wa magoli 57 na kuandaa fursa kubwa 65 , zaidi ya Rashford, Martial, Greenwood na Cavani wakati kama huo.

Sancho pia ni miongoni mwa wachezaji bora unapomlinganisha na wachezaji nyota barani Ulaya.

Tangu mwanzo wa 2018-19 , ni wachezaji saba pekee walio na magoli mengi na usaidizi zaidi ya mchezaji huyo wa England.

Kati ya wachezaji hao ni mshambuliaji wa Barcelona lionel Messi ambaye amefunga magoli 43 zaidi ya Sancho katika kipindi hicho.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post