Vita dhidi ya Corona: Tanzania imepokea dozi 1,058,400 za chanjo ya Johnson & Johnson kutoka Marekani

 

Covax

CHANZO CHA PICHA,US STATE DEPT/TWITTER

Tanzania hatimaye imejiunga na mataifa yanayotumia mpango wa kukabiliana na maambukizi ya Corona wa Shirika la Afya duniani WHO Covax ili kukabiliana na janga hilo.

Hatua hiyo inajiri baada ya taifa hilo kupokea dozi za chanjo milioni moja kutoka kwa taifa la Marekani chini ya mpango wa Covax.

Dozi hizo zipatazo 1,058,400 ni za chanjo aina ya Johnson & Johnson .

Chanjo hizo zitatumika na mahujaji, wafanyakazi wa afya, wale wa huduma za hoteli, wafanyakazi wa balozi na wagonjwa wa corona.

Katika ukursasa wake wa twitter Ubalozi wa Marekani nchini humo umesema kwamba umeikabidhi serikali ya Tanzania dozi hizo kupitia mpango wa Covax kwa ushirikiano wa Umoja wa Afrika AU .

Umeongezea kusema kuwa mpango huo ni mfano wa ushirikiano bora wa miaka 60 kati ya mataifa hayo mawili.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Balozi wa Marekani nchini humo ,Donald J Wright amesema kwamba wanasambaza chanjo hizo ili kuokoa Maisha na kuongoza ulimwengu katika harakati za kuangamiza ugonjwa huo.

Ruka Twitter ujumbe, 2

Mwisho wa Twitter ujumbe, 2

Marekani imesema kwamba hatua hiyo ni miongoni mwa mpango wa kusambaza dozi milioni 25 za chanjo katika mataifa ya Afrika.

Taarifa rasmi kutoka kwa katibu wa kudumu katika wizara ya Afya nchini Tanzania ilionukuliwa na gazeti la the Citizen nchini humo, ilisema kwamba serikali ilikuwa inatarajia kuwasili kwa aina nne za chanjo ambazo zingewasili katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne ijayo.

Wazziri wa Afya Tanzania Dorothy Gwajima kushoto

CHANZO CHA PICHA,STATE DEPARTMENT/TWITTER

Maelezo ya picha,

Wazziri wa Afya Tanzania Dorothy Gwajima kushoto

Taarifa hiyo iliotolewa wiki iliopita ilisema kwamba chanjo hiyo itaanza kupatiwa watu walio hatarini kukabiliwa na maambukizi, wafanyakazi wa afya, mahujaji , wafanyakazi muhimuna wasafiri wa mara kwa mara huku chanjo nyengine zikitarajiwa mwezi Disemba mwaka huu.

Hatahivyo kuanzia tarehe sita mwezi Julai 2021 kulingana na chombo cha habari cha The Citizen, kisiwa cha Zanzibar tayari kilikuwa kimeanza kutoa dozi ya chanjo hiyo kwa wafanyakazi wa Afya na wale walio katika hatari ya maambukizi.

Kulingana na wizara ya afya kiswani humo chanjo iliokuwa ikipewa wafanyakazi hao wa Afya ilikuwa ikifadhiliwa na serikali ya Zanzibar.

Taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa katika harakati ya kujiunga na mipango ya Corona barani Afrika tangu kifo cha aliyekuwa kiongozi wake John Pombe Magufuli ambaye amekuwa akipinga uwepo wa ugonjwa huo na tiba ya chanjo.

Hatahivyo tangu alipochukua mamlaka rais mpya Samia Suluhu Hassan ameonesha ishara kwamba amekuwa akiupa kipau mbele ugonjwa huo.

Taifa hilo ni miongoni mwa mataifa manne ya Afrika ambayo hayajaaanzisha mpango wa kitaifa kutoa chanjo kwa raia, kulingana na Kituo cha udhibiti na uzuiaji wa magonjwa Africa ACDC.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post