Checkmate:Fahamu ndege mpya ya kivita ya Urusi inayoikosesha Marekani usingizi


SERGEI KARPUKHIN

CHANZO CHA PICHA,SERGEI KARPUKHIN

Siku ya Jumanne, Urusi ilizindua ndege yake mpya ya kivita na inayoweza kufanya misheni za kijasusi ya Sukhoi "Checkmate" katika onyesho la ndege mbele ya Rais Vladimir Putin.

Habari juu ya muundo na uwezo wa ndege hii ya kivita ya kizazi cha tano ilitolewa kwenye onyesho la anga la Max-2021 lililofanyika Zhukovsky nje ya Moscow.

Ndege hii ya kivita inachukuliwa kuwa mshindani wa ndege ya kijeshi ya Marekani yenye uwezo wa kujificha F-35 na Urusi imepanga kuiuza kwa nchi nyingi ulimwenguni.

Checkmate imetengenezwa na kampuni kubwa inayomilikiwa na serikali Rostec na Shirika la Ndege la United.

Nia ya serikali ya Urusi inaonekana kuwa ni kufanya ndege hii kuwa ya kusafirishwa nje.

"Checkmate" ni nini?

Kulingana na habari zilizopo, ndege hii ya kivita ya Checkmate ni nyepesi kuliko ndege ya injini-mbili ya Sukhoi Su-57 na inaweza kubeba makombora matano ya hewani kwa safu tofauti.

Ndege hii ina uwezo wa kuzindua droni wakati ikiwa hewani na kubeba jumla ya tani 7.5 za silaha.

Checkmate inahitaji barabara fupi sana ili kupaa au kutua hiyo inachukuliwa kuwa sifa maalum ya ndege hii.

Ndege hiyo imetengenezwa kama ndege ya kivita ya kizazi kipya yenye injini moja na utumiaji teknolojia ya kisasa inahesabiwa kati ya nguvu zake kuu.

MIKHAIL SVETLOV

CHANZO CHA PICHA,MIKHAIL SVETLOV

Watengenezaji wa ndege hiyo wanasema kuwa teknolojia ya kisasa inayotumiwa katika Checkmate inafanya kazi kama rubani mwenza na itamsaidia rubani mkuu katika hali za kupigana.

Kulingana na watengezaji wa ndege hii, inaweza kupiga hadi malengo sita juu ya ardhi, hewani au baharini kwa wakati mmoja na inafanya kazi hata inapokabiliwa na usumbufu mkubwa wa kielektroniki.

Checkmate itagharimu karibu dola milioni 25 hadi 30 za Kimarekani. Baada ya majaribio ya ardhini, ndege hii itafanya safari yake ya kwanza mnamo 2023 na Urusi itaanza kuiuza kwa nchi mbali mbali kutoka 2026.

United Aircraft Corporation imesema inapanga kutengeza ndege 300 aina ya Checkmate katika kipindi cha miaka 15 ijayo. Kulingana na kampuni hiyo, idadi ya 300 imekadiriwa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wa ndege hii.

Watengenezaji wa Checkmate pia wanafanya kazi kutengeneza toleo la ndege hii ambalo halitahitaji rubani

Nchi nyingi zimeonyesha nia kuitaka "Checkmate"?

Swali muhimu ni, je India itakuwa kati ya wanunuzi wa ndege hii mpya ya kijeshi na ujasusi ya Urusi?

Hakuna habari rasmi kutoka upande wa India bado, lakini ni wazi kwamba kampuni inayotengeneza ndege hii ya kivita inaangalia India kama mnunuzi.

Watengenezaji wa Checkmate hivi karibuni walitoa video ya kionjo kabla ya kuzinduliwa kwa ndege yao. Katika video hii, marubani wa nchi nne wanaonyeshwa wakisubiri ndege mpya.

MARINA LYSTSEVA

CHANZO CHA PICHA,MARINA LYSTSEVA

Nchi hizi nne ni - Falme za Kiarabu, India, Vietnam na Argentina. Kwa sababu ya video hiyo, inakisiwa kuwa labda Urusi inaangalia nchi hizi tatu pamoja na India kama mteja anayeweza kununua Checkmate.

Lakini nafasi ya India ya kununua ndege ya kivita ya Checkmate inaonekana kuwa ndogo.

Checkmate ni ndege ya kivita ya injini moja na India tayari imeidhinisha ununuzi wa ndege 73 za kivita na ndege 10 za mazoezi za injini moja aina ya Light Combat Aircraft (LCA) Tejas Mk-1.

Ndege za Light Combat Aircraft (LCA) Tejas ni ndege ya kizazi cha nne ya injini moja iliyotengezwa India na Shirika la utengezaji wa ndege (ADA) kwa ushirikiano na Kituo cha utafiti na miundo ya ndege (ARDC) cha Hindustan Aeronautics Limited (HAL) nchini India.

LCA ilipewa jina rasmi kama "Tejas" mnamo 2003.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post