'Doomsday Torpedo': Ifahamu silaha ya 'mwisho wa dunia' ya Urusi inayoitia wasiwasi Marekani

 

The United States and Russia are also fighting for control of the seas.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

'Haiwezi kuonekana, haiwezi kuzuilika na inaweza kusababisha uharibifu mkubwa'.

Hivi ndivyo silaha aina ya Status-6 Multipurpose Ocean System inaelezewa - hii ni silaha ya Urusi ya Kinyuklia inayoitia kiwewe Marekani.

Katika vikao vyake idara ya ulinzi nchini Marekani ilisema kwamba ni mojawapo ya silaha hatari ambayo inapaswa kulishinikiza taifa hilo kuimarisha silaha zake za kiatomiki.

Wakat wa utawala wake, aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba taifa hilo linapitwa na wapinzani wake kama vile Urusi na China kwasababu ya kile alichokitaja kuwa utawala wa rais Obama uliopuuzilia mbali maendeleo ya kijeshi.

Mkutano huo unaoipatia serikali mwelekeo kuhusu silaha hatari, ulilitaja kombora hilo la kinyuklia kuwa la kujitegemea linalorushwa na manuwari ''

Mlipuko wa Kinyuklia

CHANZO CHA PICHA,US NAVY

Maelezo ya picha,

Mlipuko wa Kinyuklia

Rossikaya Gazeta, gazeti la rasmi la serikali ya Urusi lilitaja kombora hilo - kuwa 'kombora la siku ya mwisho ya dunia'.

Silaha hiyo ya Status 6 imetajwa kuwa gari linalojitegemea linaloweza kuvuka bahari ya Pasifiki na kuanzisha mashambulio hatari ya mionzi katika pwani ya magharibi ya Marekani.

Likiwa limejengwa na vifaa vinavyoliwezesha kupiga mbizi kina kirefu na kukwepa ugunduzi wa vifaa vya aina yoyote ile , silaha hiyo inabeba makombora ya kinyuklia yenye uwezo mkubwa.

''Linapolipuka linaweza kusababisha wimbi kubwa la mionzi'' , Pavel Podvig , mwanzilishi wa blogu ya Urusi kwa jina Russian Forces , aliambia BBC Mundo.

Mpango wa Urusi ni kujenga kile ambacho watalaamu wanaelezea kuwa 'silaha za wimbi la tatu'.

Manowari ya Urusi Yuri Dolgoruky.

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,

Kombora hilo ni sharti lirushwe kutoka kwa manowari

"Uharibifu mkubwa"

Hans Kristensen wa Shirikisho la wanasayansi wa Marekani anasema kwamba Marekani ina uwezo wa kuwakamata maadui zake chini ya maji lakini kombora hilo linaporushwa ''mambo yanabadilika.

"Podvig alisema kwamba iwapo kombora hilo litakamilishwa huenda likafanya uharibifu mkubwa.

Alkiyekuwa rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,

Alkiyekuwa rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin

Licha ya kuonekana kuwa tishio kubwa na idara ya ulinzi ya Marekani The Pentagon , wataalamu wana sababu nyingi za kulikosoa.

''Haijajulikana iwapo kombora hilo litaanza kutumika'', anasema Podvig..

Marekani na washirika wake waligundua kuhusu mpango wa Urusi wa kutengeneza kombora hilo wakati wa mkutano kati ya rais wa Urusi Vladmir Putin na majenerali wake katika mji wa Sochi.

Kulingana na picha zilizooneshwa na vyombo vya habari vya serikali, nakala ya siri ambayo mmoja wa wanajeshi alimuonesha Putin ilivuja.

Picha hiyo ilionesha mchoro na maelezo ya kombora hilo aina ya Status 6, lililoundwa na Rubin, mtengenezaji wa manuwari ya kinyuklia katika eneo la St. Petersburg.

Uvumi baadaye ulizuka iwapo uchapishaji wa picha hizo ulikiwa ajali ama mpango wa Urusi kutaka kuwatisha wapinzani wake.

Nakala iliokuwa na maelezo ya mradi wa kombora hilo la Status 6
Maelezo ya picha,

Nakala iliokuwa na maelezo ya mradi wa kombora hilo la Status 6

Kristensen anakumbuka kwamba Urusi imekuwa ikifanya hivyo kwa muda mrefu na hakuna uzalishaji wowote wa miradi kama hiyo ulioakamilika."

Podvig anasema: "Sidhani kombora hilo linaweza kuanza kufanya kazi kwa jinsi lilivyoelezewa. "

Kwanini basi Idara ya ulinzi ya Marekani imeliweka kombora hilo katika orodha ya silaha hatari kwa usalama wake?

''Kombora la Status 6 linawezekana kiufundi na kwa mujibu ya jamii ya majasusi , ni bora kujiandaa kwa kitu kama hicho siku zijazo'', anasema Podvig.

Hatahivyo Kristensen anapinga kwamba mfumo huo wa silaha ndio ulioishinikiza Marekani kubadilisha sera yake ya kinyuklia.

''Wametumia mfano huo kama mojawapo ya makombora yanayotishia taifa hilo ili kuweza kupata uungwaji mkono kwamba Marekani nayo inapaswa kuimarisha silaha zake za kinyuklia''.

Kombora aina ya Yars RS-24 la Urusi

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,

Wataalamu wanasema kwamba uwezo wa silaha za Marekani haujapungua

Hatari nyengine

Hatahivyo wataalamu hao wanaunga mkono madai ya Trump kwamba uwezo wa Marekani kijeshi unadidimia baada ya Urusi kutengeneza makombora mawili ambayo yanaweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine huku Marekani ikipuuza.

''Suala kwamba Urusi kwa muda sasa imekuwa ikiimarisha silaha zake , haimaanishi kwamba Marekani haikufanya hivyo, ilifanya hivyo miaka mingi iliopita'', alisema Povdig.

Sasa, baada ya miaka mingi ya sera ya kutokujilinda huko Washington, mbio hizo zinaonekana kuwa karibu kuzinduliwa upya.

"Wakati wa vita baridi, silaha za nguvu kubwa kila wakati zilitajwa ili kuwajulisha wamiliki wao; na hivyo ndivyo ilivyo kila wakati."

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post