Fahamu mataifa 10 duniani yanayotumia mapato yao kujiimarisha kijeshi

 

Ndege za kijeshi za F35 bomber ndio mradi wa kijeshi uliogharimu zaidi Marekani

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ndege za kijeshi za F35 bomber ndio mradi wa kijeshi uliogharimu zaidi Marekani

Gharama ya ununuzi wa silaha duniani ilipanda hadi $1981 billion kufikia mwaka uliopita , ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.6 kutoka mwaka 2019 kulingana na data mpya iliochapishwa na taasisi ya utafiti wa amani mjini Stockholm [SIPRI} .

Mataifa yaliotumia fedha nyingi zaidi mwaka 2020 ambayo yalitumia asilimia 62 ya fedha zote zilizotumika kununua silaha duniani ni pamoja na Marekani China India Urusi , India na Urusi.

Matumizi ya ununuzi wa silaha uliofanywa na China uliongezeka kwa mara 26 .

Mwaka 2017 Marekani ilitumia asilimia 3.1 ya mapato yake kununua silaha ikiwa ni robo ya matumizi ya taifa lililotumia fedha nyingi zaidi kununua silaha kulingana na SIPRI.

Kutokana na hilo ni wazi kwamba , Washington haipo katika mataifa 20 ambayo hutumia utajiri wao kununua silaha za kijeshi.

Hizi hapa nchi 10 ambazo zinaongoza katika orodha hiyo.

10.- Bahrain

Wanajeshi wa Bahrain wakishiriki katika mazoezi ya kijeshi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Bahrain wakishiriki katika mazoezi ya kijeshi

Bahrain ilitawaliwa na ufalme wa Madhehebu ya sunni lakini wengi wa raia wake ni Wislamu wa madhehebu ya Shiite , suala ambalo limekuwa likizua hali ya wasiwasi katika taifa hilo.

Mwaka 2011 , wakati wa mapinduzi ya Arabuni au Arab Uprising, wanajeshi wa baraza la Ghuba walipelekwa katika taifa hilo kuzuia maandamano.

Mwaka 2017 taifa hilo lilitenga $ 1,396m katika matumizi yake katika sekta ya ulinzi ikiwa ni asilimia 4.1 ya mapato yake kulingana na makadirio ya Sipri.

9.- Urusi

Mwaka 2017, Urusi kwa mara ya kwanza ilipunguza matumizi yake ya ununuzi wa vifaa vya kijeshi tangu 1998 ikishusha matumizi yake kwa asilimia 20 na kufikia $ 66,335m ikiwa ni sawa na asilimia 4.3 ya pato lake la nchi.

Silaha ya kujilinda dhidi ya makombora nchini Urusi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Silaha ya kujilinda dhidi ya makombora nchini Urusi

Kulingana na Siemon Wezeman, mchunguzi mkuu katika taasisi ya SIPRI , punguzo hilo linatokana na matatizo ya kiuchumi ambayo taifa hilo limekuwa likishuhudia tangu 2014 , kwasababu kuliimarisha jeshi lake kufikia viwango vya kisasa kumekuwa kipao mbele cha Moscow..

8.- Lebanon

Kati ya mataifa kumi yalio na mzigo wa kijeshi duniani , mataifa sita yanatoka eneo la mashariki ya kati . Na taifa la Lebanon ni miongoni mwao.

Taifa hilo lilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1975 na 1990 na tangu wakati huo maisha yake ya kisiasa yamekumbwa na mgawanyiko mkubwa.

Sera yake ya nyumbani na ile ya kigeni imeshawishiwa na majirani zake Syria, pamoja na nguvu ya kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Hezbollah ambalo mwaka 2006 lilipigana vita dhidi ya Israel.

Matumizi yake ya kijeshi yalifikia $ 2,441m sawa na asilimia , 4.5% ya pato lake.

7.- Israel

Tangu lilipoanzishwa 1948, taifa la Israel limezungukwa na maataifa inayodai kuwa maadui zake .

Hali hiyo ilirekebishwa baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani na Misri 1979 na Jordan 1994.

Silaha ya kujilinda dhidi ya makombora Israel

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Silaha ya kujilinda dhidi ya makombora Israel

Hatahivyo taifa hilo bado linaendelea kuwa na maadui hususan katika mpaka wake na Syria pamoja na wapiganaji wa Lebanon wa Hezbollah ambao ni washirika wa Iran, mojawapo ya mataifa ambayo hayaonani macho kwa macho na Israel.

Kulingana na Sipri , jeshi la Israel kufikia mwaka 2017 lilikuwa likitumia $ 16,489m ambazo ni aslimia 4.7%ya pato lake .

6.- Jordan

Jordan ilijipatia uhuru wake 1946 na tangu wakati huo imekumbwa na hali ya wasiwasi kutokana na mazingira ya mzozo.

wMwaka 1967, wakati wa vita vya siku sita dhidi ya Israel, taifa hilo lilipoteza eneo la West Bank na Jerusalem maeneo ambayo ilikuwa ikiyamiliki tangu vita vya Waarabu na Israel 1948.

Mwaka 1984, alitia saini makubaliano ya amani na Israel hatua ambayo haimkingi na tatizo la usalama linaloendelea kukumba eneo hilo , kama lile linalosababishwa na Islamic State.

Mwaka 2017, lilitenga $ 1,939m katika sekta ya ulinzi ikiwa ni sawa asilimia 4.8% ya pato lake la nchi..

5.- Algeria

Taifa la Algeria limekumbwa na vipindi vikali vya ghasia katika historia yake kama taifa huru ambavyo vilianza 1962.

Baadhi ya vipindi hivi vimetokana na hali ya wasiwasi kati ya makundi ya kidini na yale ya kidunia ya jamii yake.

Kiongozi wa zamani wa al - Qaeda wa maghreb

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,

Kiongozi wa zamani wa al - Qaeda wa maghreb

Kati ya 1992 na1998, taifa hilo lilikumbwa na mzozo wa ndani kwa ndani ambao ulisababisha zaidi ya vifo 100,000 baada ya kufutiliwa mbali kwa uchaguzi ambapo kundi la Islamic Salvation lilionekana kana kwamba litaibuka mshindi.

Tangu wakati huo , taifa hilo limeendelea kuathiriwa na ghasia za Kiislamu , lakini pia limekumbwa na mashambulio kutoka kwa makundi ya wapiganaji kama vile lile la Al Qaeda kutoka Islamic Maghreb.

Mwaka 2017, liliandikisha matumizi ya yanayokadiriwa na Sipri kuwa $ 10,073m ikiwa ni sawa na 5.7% ya pato lake la taifa .

4.- Kuwait

Likiwa na ardhi yenye ukubwa wa kilomita 17,818 na chini ya watu milioni Kuwait ni taifa dogo lililozungukwa na majirani: Saudi Arabia, Iran na Iraq.

Taifa hilo linamiliki kambi kadhaa za Marekani ambapo baadhi ya majeshi ya muungano wa kimataifa unaopigana dhidi makundi ya kundi la Islamic State yanaishi.

Mwaka 2017, lilitenga matumizi ya $ 6,831m, sawa na asilimia 5.8% ya pato lake.

Siku ya kimataifa ya maonesho ya silaha Kuwait

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Siku ya kimataifa ya maonesho ya silaha Kuwait

3.- Congo

Likitumia asilimia 6.2 ya pato lake katika vifaa vya kijeshi , Jamhuri ya Congo ndio taifa la Afrika linalotenga utajiri wake mkubwa katika sekta ya ulinzi likitenga $ 484m kulingana na makadirio ya Sipri.

Taifa hilo limeshuhudia vipindi kadhaa vya mizozo ya ndani kwa ndani chini ya uongozi wa Denis Sassou-Nguesso, mwanajeshi wa zamani ambaye alitawala taifa hilo kati 1979 na 1992 na ambaye alirudi madarakani 1997 na ambaye amesalia hadi sasa .

2.- Saudi Arabia

Tangu 2015, serikali ya Saudia imeongoza kundi la mataifa katika vita vya Yemen dhidi ya waasi wa Houthi ambao wanaungwa mkono na Iran.

Wanajeshi wa Yemen

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Tukio hilo ni mojawapo ya baadhi ambapo Riyadh na Tehran zinapigania udhibiti wa kisiasa, na kiuchumi wa eneo zima la mashariki ya kati .

Ufalme wa Saudia pia hushiriki katika muungano wa kimataifa dhidi ya kundi la Islamic State. Kulingana na Sipri taifa hilo lilitenga $ 69,413m sawa na asilimia 10 ya pato lake.

1.- Oman

Likiwa katika eneo la kimkakati la mkondo wa Hormuz , mojawapo ya maeneo muhimu ambayo meli za mafuta hupita na likiwa na majirani kama vile Iran, Saudi Arabia na Yemen ,Ufalme wa Oman umeongeza matumizi yake ya kijeshi katika kipindi cha miongo kadhaa iliopita.

Ukweli ni kwamba ndilo taifa duniani ambalo hutumia fedha nyingi katika kitengo chake cha ulinzi. Mwaka 2017, taifa hilo lilitenga $ 8,686m sawa na asilimia 12% ya pato lake .

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post