‘Kiuno cha nyigu’’, nyonga na makalio makubwa, ngozi nyororo... unapotizama picha kwneye mitandao ya kijamii, wakati mwingine ni vigumu kufahamu ni picha ipi imehaririwa na ile ambayo ni halisi.
Lakini je mtuma picha angekuwa anatoa maelezo kwamba picha hii imefanyiwa uhariri na hii ni halisi ingewasaidia watumiaji kujiamini?.
Sheria mpya nchini Norway sasa inaanza kutekelezwa ambayo itamaanisha kuwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wenye ushawishi hawatatuma picha zazo zilizohaririwa bila kusema ni nini wamezifanyia picha zao.
Sheria hii itazihusu jumbe zote za picha zilizplipiwa kwenye majukwa yote ya mitandao ya kijamii, kama sehemu ya juhudi za"kupunguza shinikizo za miili yao’’ambazo watumiaji wa mitandao vijana wanazipata wanapowatazama watu wenye ushawishi kwenye mitandao hiyo.
Madeleine Pedersen, 26, ni mshawishi katika mtandao wa Instagram kutoka Moss nchini Norway.
Anasema "umefika wakati " sheria zibadilishwa na anatumaini sheria hiyo itawazuia vijana kujilinganisha na picha ambazo sio halisi.
"Kuna watu wengi sana ambao wameshindwa kujiamini kutokana na miili yao au uso wao,"anasema.