Hizi ni nchi tano zenye wafungwa wachache zaidi duniani

 

Jail

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kuna zaidi ya watu milioni 11 wako magerezani duniani kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni iliyochapishwa na World Prison Population List (WPPL), katika utafiti wa Taasisi ya utafiti ya Criminal Policy Research (ICPR), ya Chuo Kikuu cha London, Birkbeck.

Marekani inaelezwa kuwa na wafungwa karibu robo ya wafungwa wote duniani, huku idadi ya wafungwa ikiongezeka kwa asilimia 68% katika nchi ya Cambodia, 61% huko Nicaragua na ongezeko la asilimia 53% kwa nchi ya Misri.

Pamoja na idadi hiyo ya wafungwa kuonekana kubwa na ikiongezeka katika baadhi ya nchi, zipo baadhi ya nchi duniani ambazo wafungwa wako wachache.

BBC

1: San Marino

Jamhuri ya San Marino ni nchi ndogo iliyo milimani karibu na pwani ya Italia. Ni moja ya nchi tajiri kwa kigezo cha pato ghafi la mwaka. Nchi hiyo yenye idadi ndogo ya watu ambao ni takribani 40,000.

Ina gereza moja tu rasmi kwa viwango vya kuitwa gereza, ukiacha vituo vya muda vya urekebisha tabia katika baadhi ya maeneo hasa vilipo vituo vya Polisi.

January 2020, nchi hiyo ilikuwa na wafungwa wawili tu waliokuwa wanatumikia vifungo jela. Watuhumiwa wengi wanaokutwa na hatia ya kutenda uhalifu na mahakama hutumikia vifungo vyao katika jela za Italia. Wafungwa hao wawili baadae waliachiwa April 15.

April 26, 2020 mfungwa pekee katika jela huko San Marino aliwekewa maktaba binafsi, chumba cha mazoezi (gym) na Televisheni, ili kumfanya asiwe mpweke zaidi.

Kutokuwepo kwa wafungwa ama kuwepo kwa wafungwa wachache kunatajwa ni kwa sababu kuwepo kwa visa vichache vya uhalifu kwa sababu utajiri wa nchi hiyo na idadi ndogo ya watu.

2: Liechtenstein

BBC

Hii ni nchi nyingine ndogo na yenye watu wachache wasiofikia 40,000 kwa mujibu wa makadirio ya watu ya mwaka 2019.

Ripoti ya World Prisons Brief (WPB) inaonyesha nchi hiyo ina gereza moja la uhakika lenye uwezo wa kuchukua wafungwa wasiozidi 20. Kumekuwa na wafungwa wachache sana gerezani. Wale wanaohukumiwa vifungo vya kwenda jela kwa kipindi cha miaka zaidi ya miwili hupelekwa Australia kutumikia vifungo vyao.

Katika miaka 10 iliyopita mwaka pekee uluioshuhudiwa nchi hiyo kuwa na wafungwa wengi zaidi ulikuwa mwaka 1997 ilipokuwa na wafungwa 75.

Kwa mujibu wa mtandao wa Mentalfloss nchi inatajwa kuwa na kiwango kidogo cha matukio ya uhalifu, huku kisa cha mwisho cha mtu kuuawa na kubainika ilikuwa mwaka 1997. Kutokana na kuwa na visa vichache sana vya uhalifu, ni kawaida wananchi kulala bila hofu ya kufunga milango na madirisha ya nyumba zao au kutembea nyakati za usiku.

Tuvalu

Tuvalu

CHANZO CHA PICHA,GIGAZINE

Tavalu, ni kisiwa kinachopatikana Kusini mwa Bahari ya Pasific. Ni kisiwa huru ndani ya Jumuiya ya Madola chini ya Uingereza. Kinaundwa na visiwa vidogo 9, vikiwa na watu wachache wasiozidi 15,000. Visiwa hivi viko katikati ya Hawaii na Australia.

Kwa mujibu wa mtandao wa prisonstudies kati ya mwaka 2000 mpaka mwaka 2012, Tuvalu ilikuwa na wafunga 36 tu nchi nzima, ambapo mwaka 2012 ikiwa na idadi kubwa kabisa ya wafungwa wapatao 12. Mwaka 2007 ilikuwa na wafungwa watatu tu katika kipindi cha mwaka mzima. Kutokana na udogo wa visiwa vyake na uchache wa watu, ujamaa na kufahamiana kumekuwa kwa karibu zaidi kunakosaidia kupunguza uhalifu.

Andorra

Andorra

CHANZO CHA PICHA,PRISON INSIDER

Kama zilivyo nchi nyengine ndogo ambazo zina magereza machache, Andorra ni miongoni mwao, ina gereza moja kubwa linaloitwa La Comella lenye uwezo wa kuchukua wafungwa wasiozidi 150, kwa mujibu wa Ripoti ya World Prisons Brief (WPB) ya mwaka jana.

Pamoja na ukubwa huo, gereza hilo halijawahi kujaa, mara nyingi huwa na wafungwa wa wastani wa kati ya 30 mpaka 60 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Baraza la Ulaya, mpaka April 15 Mwaka 2020 nchi hiyo ya Andorra ilikuwa na wafungwa 43 tu.

Nauri

Google

CHANZO CHA PICHA,GOOGLE

Ni kisiwa kidogo kaskazini mashariki mwa Australia. Benki ya dunia ilikadiria nchi hiyo kuwa na watu 12,500 mwaka 2019. Mpaka mwaka 2014 ilikuwa na gereza moja tu la wafungwa.

Mtandao wa prisonstudies kupitia ripoti ya mwaka jana ya World Prisons Brief (WPB) umeandika kwamba kati 2003 mpaka mwaka 2012, nchi hiyo ilikuwa na wafungwa wasiozidi 70. Katrika miaka hiyo tisa ni mwaka 2009 pekee uliokuwa na wafungwa wengi, wapatao 37, lakini miaka mingine imekuwa na wastani wa wafungwa 6 mpaka 26.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post