Olimpiki Tokyo:Video Bondia amng'ata sikio mpinzani wake akijaribu kutafuta ushindi wa dakika za mwisho

 

Youness Baalla na David Nyika

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kabla ya kutekeleza kitendo hicho bondia huyo alikuwa amekabiliwa na makonde makali

"Niliumwa mara moja katika mashindano ya mataifa ya jumuiya ya madola , lakini tafadhali haya ni mashindano ya Olimpiki."

Yule ambaye hashangazwi ni bondia wa New Zealand David Nyika. Na aliyejaribu kumn'gata alikuwa bondia wa Morocco Youness Baalla.

''Na jina lililojiri katika fikra zangu kwa wale wote walioshuhudia pigano hilo la uzani mzito mjini Tokyo, na wale ambao hawajawacha kuitazama kanda hiyo ya video katika mitandao ya kijamii ni lile la Mike Tyson''.

Miaka 24 iliopita, Tyson alimng'ata sikio Evander Holyfield katika pigano la uzani mzito zaidi duniani 1997.

Matokeo yake - Tyson alipigwa marufuku na kupoteza leseni yake ya ndondi kwa takriban miezi 15.

Bado haijulikani iwapo Baalla atawekewa vikwazo ambapo katika pigano lao la raundi ya mwisho alijaribu kumng'ata mpinzani wake.

Tukio hilo halikukubalika na refa na ijapokuwa raia huyo wa Morocco aliweza kumaliza pigano hilo alishindwa kwa pointi tano kwa sufuri.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

"Nilimwambia Kitu"

"hakuweza kuniuma kabisa kwasababu alikuwa amevalia kifaa cha mdomoni na pia nilikuwa natokwa na jasho'', Nyika alielezea pogano hilo.

Kanda hiyo ya video inaonesha juhudi za bondia huyo wa New Zealand za kuondoa kichwa chake kutoka kwa mdomo wa mpinzani wake , huku mmoja ya waandishi wa habari wakielezea malengo ya Baalla kama kitendo cha mtu mwenye wazimu."

"Sikumbuki nilimwambia nini , lakini kuna kitu nilimwambia'' , aliongezea Nyika, ambaye alifuzi hadi robo fainali," .

Kulingana na habari za maafisa kutoka kwa michezo ya Olipiki ya , Younnes Baalla ,22 alizaliwa Casablanca.

Alifuzu katika michezo ya Olimpiki kutokana na mchezo wake mzuri katika michuano ya kufuzu ya Afrika iliofanyika mjini Dakar Senegal , mwaka uliopita.

Mkufunzi wake alikuwa raia wa Cuban Dagoberto Rojas Scott.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post