"Niliamua kulipiza kisasi cha kifo cha mume wangu kwa kuanzisha urafiki na mtu aliyemuua, nikafunga nae ndoa na hatimaye nikalipikiza kisasi."
Mwanamke mmoja, mkazi wa Wilaya ya Bajaur, nchini Pakistan, alikamatwa na Polisi na kupelekwa mahakamani, kabla ya kupelekwa jela ya Chakdara
Mwanamke huyo anasema alijaribu kwa miaka mitatu kulipiza kisasi kutokana na kifo cha mume wake, na alifanya mipango madhubuti kutekeleza hilo.
Wilayat Khan, mpelelezi katika kituo cha Polisi cha Louisim, Inayat Fort huko Bajaur, aliiambia BBC kwamba kesi hiyo ilikuwa ngumu, lakini alijaribu na kufanikiwa.
Mume wa mwanamke anayetuhumiwa, Shah Zameen alifariki miaka mitatu iliyopita, lakini haifahamiki wazi kifo chake kilitokana na nini, aliuawa ama alifariki kifo cha kawaida. Lakini mtuhumiwa anadai alipata taarifa kutoka kwa watu binafsi kwamba mumewe aliuawa kwa kuchomwa sindano ya sumu, na aliyemuua ni Gulista, aliyekuwa rafiki wa karibu wa mumewe.
Hata hivyo hakuna taarifa za kifo cha mumewe zilizoripotiwa kwenye kituo cha Polisi. Polisi wanasema wakati huo hakukuwa na kituo cha Polisi karibu na hakuna nyaraka zozote zinazohusu kifo cha mtu huyo, hali inayoleta mashaka pia huenda Shah Zameen ameuawa.
Kwa mujibu wa Polisi, siku mbili baadaye walipata taarifa kwamba mtu anayeitwa Gulistan ameuawa kwa kupigwa risasi.
Mkuu wa Polisi wa eneo hilo Vilayat Khan aliwaamuru Polisi waliokuwepo eneo la tukio kwamba, wahakikishe hakuna mtu anayeondoka kwneye eneo hilo, akiwa njiani kurejea.
"Nilipofika, kulikuwa na maiti iliyotapakaa damu, alipigwa risasi moja kichwani na nyingine upande wa kulia wa mwili wake. Wakati huo mtuhumiwa mwanamke akiwa amekaa kando ya maiti hiyo. watu walikusanyika kwa wingi ndani na nje ya nyumba," Wilayat Khan alisema. "Tuliwaweka watu kando na kuanza kufanya uchunguzi na kukusanya ushahidi kwenye eneo la tukio."
Mwanamke anayependana na Mkimbizi wa Afghan, Shah Zameen
Kwa mujibu wa taarifa za Polisi , mwanamke huyo alisema mumewe wa kwanza aliyeuawa alikuwa ni mkimbizi kutoka Afghanistan akiiishi katika jimbo la Kunar, Afghanistan. Mumewe alikuwa akifanya kazi Peshawar na waliishi maisha ya furaha, wakijaaliwa kupata binti mmoja.
Kwa mujibu wa Polisi, mtuhumiwa huyo alieleza katika maelezo yake, "Mume wangu alikuwa na urafiki wa karibu sana na Gulistan. Mume wangu alikuwa akimtumia Gulistan kusimamia shughuli zake ikiwemo pesa huko Peshawar. Mume wangu na Gulistan walikuwa marafiki wa karibu sana. "
Mwanamke huyo anaeleza kwamba siku moja mumewew alirudi nyumbani akisema hajisikii vizuri, na kumuomba Gulistan kwamba anatakja pesa, lakini Gulistan hakumpatia akisema hakuwa na pesa kwa wakati huo.
Kwa mujibu wa Vilayat Khan, mtuhumiwa huyo alieleza, "Gulistan, baada ya kumpa pesa mume wangu, alisema kama una umwa nitakuletea dawa kutoka Inayat Kali Bazaar." Gulistan akaja na sindano mbili na vidonge. Akachoma moja, ilikuwa nje ya nyumbani akisema sindano ya pili atachoma nyumbani na kunywa vidonge, na atapata nafuu.
"Baada ya sindano, hali ya mume wangu ikabadilika na kuwa mbaya zaidi na kudondoka chini. Watu waka na kumpeleka hospitali, lakini baadae alifariki," alisema katika maelezo yake aliyotoa Polisi.
Mpango wa kulipiza kisasi
Mwanamke huyo aliiambia Polisi kwamba, alipojaribu kuuliza watu kuhusu mazingira ya kifo cha mumewe, walimuelezwa kwamba, kwa mazingira yalivyo, rafiki wa mumewe Gulistan atakuwa amemuua kwa kutumia zile sindano za sumu, kwa sababu baada ya kuchomwa hizo sindano ndio hali ikabadilika.
Baada ya kupata hizo taarifa ndio ulikuwa wakati hasa alipoamua na kukata shauri ya kulipiza kisasi cha kifo cha mumuewe..
Kwa mujibu wa Polisi, mwanamke huyo alitumia miezi sita kujaribu kulipiza kisasi, lakini ilishindikana, akaamua kuangalia njia nyingine (Plan B), ambayo ilikuwa ni kujiweka karibu zaidi na Gulistan ili alipize kisasi.
Ingawa Gulistan Khan, alikuwa ameoa na ana mtoto mmoja wa kiume, mwanamke huyo akaamua kumtumia meseji ukaribu ukaanza na baadae wakaoana, ingawa kwa kutumia njia ya kumrubuni kimapenzi.
Mwanamke huyo aliiambia Polisi kwamba, alimrubuni Gulistan kwa kumwambia ana pesa, anaweza akatumia kununulia gari ambalo anagelitumia kwneye shughulio zake na wakaishi maisha ya furaha.
Wakati wa sikukuu ya Eid kubwa mwaka uliopita, walifunga ndoa na kukaa kwenye nyumba ya dada yake na Gulistan. Lakini kwa sababu alikuwa na lengo lake, mazingira yale yasingekuwa rafiki kutekeleza azma yake ya kulipiza kisasi, akamuuuliza mumewe watakaa pale mpaka lini?
Mwanamke huyo, ambaye sasa ni mke wa Gulistan, aliyekuwa rafiki wa mumewe na anayemshuku kumuua mumewe, alimshawishi mumewe na wakapanga nyumba huko Inayat Kali, lakini kwa sababu alikuwa na dhamira yake, akamueleza mume wake mpya Gulistan (Anayemtaja kama muuaji wa mumewe) kwamba kwa sababu wanaishi peke yao, na wakati mwingine anabaki peke yake nyumbasni, mumewe akienda kwenye mihangaiko, usalama ni mdogo na wanaweza kuvamiwa na wezi, ni muhimu kununua silaha ya kujilinda.." Alinunua bastola kwa dola 180. "Ilisema ripoti ya Polisi.
"Ni miaka mitatu tangu mume wangu afariki na miaka miwili nikiwa najaribu kutafuta namna gani ya kulipiza kisasi na lini. Nilikuwa natafuta fursa ya kutumia bastola akirudi nyumbani," alisema, kwa mujibu wa Polisi.
Siku ya tukio la Kulipiza Kisasi
Akirejea siku ya tukio la kulipiza kisasi, alisema, "Nilikuwa macho usiku na kwenda chumbani muda kama wa saa saba usiku, wakati huo Gulistan alikuwa amelala. "
Alienda katika chuba alicholala Gulistan na kumtandika risasi ya kwanza kichwani na ya pili kulia mwa mwili wake. Bada ya kutwekeleza mauaji hayo ya kulipiza kisasi, hakukimbia alikaa kando ya maiti ya Gulistan mpaka kulipopambazuka. Baada ya kupambazuka na watu kujaa aliwaambia kwamba kuna mtu amemuua mumewe (Gulistan ) kwa risasi kabla ya taarifa kutolewa na Polsii kufika katika eneo la tukio.
Ofisa wa Polisi Vilayat Khan alisema mwanamke huyo aliendelea kung'ang'ania kwamba hajahusika na kifo cha mtu huyo, lakini baadae baada ya uchunguzi wa Polisi alikuja kukiri kutekeleza mauaji hayo na kueleza kila kitu mpaka alipoificha bastola. Polisi waliichukua bastola hiyo, huku mtoto wa Gulistan akishuhudia kila kitu.
Wananchi wanasema Gulistan alikuwa mtu mzuri, akifanya shughuli zake vyema katika maeneo ya karibu na nyumbani. Polisi walisema mwanamke huyo yuko jela kwa sasa baada ya kufikishwa mahakama